Main Article Content

Kiswahili katika matamasha ya maigizo ya shule na Vyuo Nchini Kenya


Mosol Kandagor
Toboso Mahero

Abstract

Matamasha ya shule na vyuo nchini Kenya huandaliwa kila mwaka kati ya Januari na Aprili. Matamasha haya hushirikisha kila shule na  vyuo vya serikali pamoja na vya binafsi. Matamasha haya yalianzishwa mwaka wa 1959. Huu ulikuwa wakati wa ukoloni na kwa sababu  hii, maigizo yalitawaliwa na sifa za matamasha na maigizo ya Uingereza yaliyoshirikisha taasisi za elimu ya juu. Matamasha ya mwanzo  mwanzo nchini Kenya yalishirikisha taasisi za Wazungu na Wahindi pekee. Baada ya uhuru, matamasha haya yalianza kushirikisha shule  na taasisi za Kiafrika. Ingawaje lugha za Kiafrika zimekubaliwa kushirikishwa katika tungo za kuwasilishwa katika matamasha haya, mawasilisho mengi huwa katika lugha ya Kiingereza. Hali hii imewacha Kiswahili na lugha nyingine za Kiafrika zikikosa kushirikishwa  kikamilifu. Makala basi inajadili nafasi ya Kiswahili katika ujenzi wa taifa kupitia kwa matamasha haya. 


Journal Identifiers


eISSN: 2683-6432
print ISSN: 2683-6440