Main Article Content

Suala la upole katika fasihi andishi: Uchanganuzi katika riwaya ya Pendo la Karaha (2014)


Agnes Mueni Muteti
Evans M. Mbuthia
Mary Ndung'u

Abstract

Makala hii inajadili suala la upole linavyojitokeza katika riwaya ya Pendo la karaha iliyoandikwa na John Habwe (2014). Misingi ya riwaya  hii imejielekeza katika ukiukaji wa ukawaida ulioko katika jamii. Vijana wanatamani nafasi za kazi ughaibuni. Wanapofika huko,  wanakumbana na changamoto nyingi na matarajio yao hayafikiwi. Kudra, bintiye Riziki na mhusika mkuu, anakata tamaa kutokana na  kauli anazopokezwa na wanaomzunguka; naye Kassim anakata tamaa kutokana na vitendo anavyotendewa na mamaye, Rehema.  Nadharia inayoongoza mjadala huu ni nadharia ya upole iliyoasisiwa na Brown & Levinson (1987). Makala inabainisha kauli zenye upole  zinazotamkwa na wahusika mbalimbali, kuchunguza mikakati ya upole inayoteuliwa na wahusika katika mawasiliano yao na kutambua  matendo yanayochangia kuwapo kwa upole katika mawasiliano baina ya wahusika. Kutokana na data zilizokusanywa, inaweza kuhitimishwa kuwa upole si suala la kiakademia tu, bali linaweza kuwa na umuhimu katika safu ya udiplomasia na katika masuala ya  amani na maridhiano miongoni mwa wanajamii katika mataifa yetu na hata kimataifa. 


Journal Identifiers


eISSN: 2683-6432
print ISSN: 2683-6440
 
empty cookie