Main Article Content

Lugha mkakati katika mawasiliano ya Chokoraa


Ruth M. Binyanya
Ayub Mukhwana
Samuel M. Obuchi

Abstract

Makala hii inachunguza matumizi ya lugha mkakati katika mawasiliano ya chokoraa. Chokoraa huishi mitaani na hupitia changamoto  mbalimbali zikiwamo unyanyapaa na ukosefu wa chakula. Kwa hali hii basi, chokoraa hufanya kazi kama vile kuwabebea wafanyabiashara  wadogo bidhaa za kuuza na kuosha magari. Vile vile, chokoraa, wakati mwingine, huomba msaada kutoka kwa  wanakundi-nje. Hali hizi mbalimbali ndizo huwafanya chokoraa kutumia lugha mkakati na kwa mitindo mbalimbali ili kutimiza nia zao za  wakati husika. Data iliyokusanywa kuhusiana na mada hii inaonesha kuwa chokoraa hutumia lugha kutegemea muktadha wa  mawasiliano. Tumebaini kuwa chokoraa hutumia lugha mkakati kwa kutumia mbinu kama vile kuchanganya ndimi, uradidi, matumizi ya  majina yanayorejelea Mungu na vile vile matumizi ya lugha ya matusi kwa nia ya kupambana na unyanyapaa kutoka kwa wanakundi-nje.  Kwa kufuata mkabala wa isimujamii, makala hii inaonesha kuwa chokoraa hutumia lugha mkakati ili kukidhi mahitaji yao ya wakati  husika. Makala hii ni ya uchambuzi ubora na hivyo basi yalitumia data ambayo ilituwezesha kushughulikia mada hii. Data ambayo  imetumiwa katika makala hii ilikusanywa na Ruth Binyanya baina ya Januari-Agosti, 2020 mtaani Mathare, jijini Nairobi kwa ajili ya tasnifu  yake ya uzamivu ambapo alishughulikia matumizi ya lugha mkakati katika kutimiza nia mbalimbali za wanafamilia wa mitaani. 


Journal Identifiers


eISSN: 2683-6432
print ISSN: 2683-6440