Main Article Content

Uainishaji wa mofimu katika sentensi za kiswahilikiingereza


Shadrack Kirimi Nyagah
Iribe Mwangi
Basilio Gichobi Mungania

Abstract

Makala hii inalenga kuainisha mofimu katika sentensi zinazotokana na uhamishaji msimbo unaohusu lugha za Kiswahili na Kiingereza.  Utafiti huu unaongozwa na Modeli ya Kiunzi cha Lugha Msingi ya Myers-Scotton (1993) na modeli ya M-4 ya MyersScotton & Jake (2000).  Kando na kuainisha mofimu katika sentensi za KiswahiliKiingereza, kazi hii pia inachunguza majukumu yanayotekelezwa na lugha za  Kiswahili na Kiingereza katika sentensi moja. Data ya utafiti huu imetokana na mazungumzo ya kawaida kutoka katika vipindi viwili  vinavyoigizwa kwenye runinga ya NTV- Kenya ambavyo ni “The Wicked Edition” na “The Real Househelps of Kawangware.” Matokeo ya  uchunguzi huu yanadhihirisha kwamba mofimu katika sentensi za KiswahiliKiingereza zinaweza kuainishwa katika matapo manne  makuu, yaani: mofimu za kidhana, mofimu za kimfumo za mapema, mofimu mfumo za kidaraja na mofimu mfumo za nje. Kila aina ya  mofimu hutekeleza jukumu mahususi. Hali kadhalika, lugha ya Kiswahili na ya Kiingereza huwa na uamilifu tofauti hivi kwamba lugha ya  Kiswahili huitawala lugha ya Kiingereza kwa kuiwekea muundo wa kimofosintaksia ambamo mofimu za Kiingereza huchopekwa.    


Journal Identifiers


eISSN: 2683-6432
print ISSN: 2683-6440