Main Article Content

Michakato ya kifonolojia inayoathiri irabu katika muundo wa vivumishi vya lugha za mnyambuliko: Mifano kutoka kiimenti


Kenneth Kinyua Thuranira
James Ontieri
Nancy Ayodi

Abstract

Kivumishi ni kipashio muhimu katika lugha kinachotumika pamoja na maneno mengine kufanikisha mawasiliano. Utafiti wa kifonolojia  kuhusu kategoria mbalimbali za maneno ya lahaja za lugha ya Kimeru umewahi kufanywa. Kwa mfano, Wa Mberia (1981; 1993; 2002;  2015), Gacunku (2005) na Maore (2013) ni miongoni mwa wataalamu waliochanganua masuala ya kifonolojia katika lahaja mbalimbali za  Kimeru. Hata hivyo, hatukupata utafiti uliochunguza muundo wa kivumishi cha lahaja ya Kiimenti ukiangazia michakato ya kifonolojia  inayokumba kategoria hii ya maneno. Kwa hivyo, makala hii itanachunguza michakato mahususi ya kifonolojia inayokumba irabu pekee  katika muundo wa kivumishi cha Kiimenti. Hii ni kwa sababu kivumishi cha Kiimenti hupitia mabadiliko mengi ya sauti kutoka muundo  wake wa ndani hadi muundo wa nje. Aidha, makala hii inafafanua sheria zinazodhibiti mabadiliko hayo. Nadharia ya Fonolojia Zalishi  Asilia (FZA) ya Hooper (1976) imetumika kuchanganua data katika makala hii. Data iliyochanganuliwa ilipatikana maktabani na uwandani.  Maktabani, kazi mbalimbali zilizoangazia vivumishi vya Kiimenti zilichambuliwa. Utafiti wa uwandani ulifanyika katika wadi ya  Abothuguchi Magharibi kwenye Kaunti ya Meru ambapo miktadha ya mikutano ya masoko, shule na makanisa iliteuliwa kimakusudi ili  kukusanya data kuhusu vivumishi mbalimbali kutoka kwa wazungumzaji wazawa wa lahaja ya Kiimenti. Utafiti ulibainisha kuwa kuna  michakato mingi ya kifonolojia inayopatikana katika vivumishi vya Kiimenti. Michakato hiyo huathiri irabu na konsonanti katika muundo  wa vivumishi vya lahaja husika. makala hii itakuza na kuendeleza usomi wa vivumishi katika lugha mbalimbali za Kiafrika. Uelewa wa  michakato ya kifonolojia inayoathiri irabu utasaidia kueleza kikamilifu muundo wa vivumishi vya Kiimenti na kuchochea utafiti zaidi  kuhusu  muundo wa vivumishi katika lugha za Kiafrika.


Journal Identifiers


eISSN: 2683-6432
print ISSN: 2683-6440
 
empty cookie