Main Article Content

Udhihirikaji wa mamlaka na mahusiano yaliyo na ubishi kupitia dhamira na namna katika usemi


Teresia W. Waweru
John Habwe
Iribe Mwangi

Abstract

Makala inahusu dhamira na namna katika usemi na udhihirikaji wa mamlaka na mahusiano yanayowezeshwa kutokana na matumizi ya  lugha ya Kiswahili katika kanisa Katoliki kwenye nyumba za watawa za malezi. Kanisa Katoliki ni mojawapo ya asasi zenye desturi, sheria, itikadi, imani na kanuni zinazoliongoza. Uongozi wake hutekelezwa kutegemea ngazi zilizoko. Mojawapo ya viungo muhimu vya kanisa ni  jamii ya watawa wenye viongozi katika mashirika kama Mama Mkuu, Makamu wa Mama Mkuu, Wasaidizi wa Mama Mkuu (washauri),  viongozi wa maeneo na walezi. Aidha, kuna watawa walioweka nadhiri za daima, nadhiri za muda na walelewa. Watawa hutumia lugha ya  Kiswahili katika mitagusano inayozalisha mahusiano kati yao. Kila lugha hudhihirisha itikadi na mamlaka na hutegemea nafasi ya  mshirika katika asasi fulani kama nafasi ya kiongozi, daktari na washirika kudhihirisha lugha ya mamlaka waliyonayo (Fairclough, 1992).  Ngazi za kiutawala kwa watawa zinadhihirisha mamlaka yaliyopo ya kitawa kupitia matumizi ya lugha ya Kiswahili katika usemi. Kutokana  na hoja hii kulidhihirika ubishi katika mahusiano ya kimamlaka wakati wa mawasiliano baina ya walezi na walelewa katika usemi kupitia  matumizi ya lugha ya Kiswahili (Wodak, 2001). Data zilikusanywa nyanjani katika nyumba za kitawa katika Jimbo Kuu la Mombasa katika  Shirika la Masista wa Mt. Yosefu ambapo lugha ya Kiswahili hutumika kwa mapana. Matini hizi ziliangaliwa katika kiwango cha kishazi na  sentensi kupitia dhamira na namna kwa mtazamo wa Sarufi Amilifu Msonge. Nadharia hii inajihusisha na wazo la uamilifu wa lugha. Je,  kuna uwezekano wa ubishi wakati wa mawasiliano kati ya walezi na walelewa kwenye nyumba za watawa za malezi? Je, mamlaka na  mahusiano hudhihirika vipi katika matumizi ya lugha yaliyo rasmi na yasiyo rasmi katika nyumba za watawa za malezi? Maswali haya  ndiyo yalijibiwa katika makala. 


Journal Identifiers


eISSN: 2683-6432
print ISSN: 2683-6440
 
empty cookie