Main Article Content

Sintaksia Ya Kirai Kijalizo Na Uchopoaji Wa Viambajengo Katika Kiswahili


Joseph Wanyonyi Mulalu
Mosol Kandargor
Mary Lonyangapuo

Abstract

Kazi hii imeshughulikia sintaksia ya Kirai kijalizo (Kkijzo) na uchopoaji wa viima katika sentensi za Kiswahili. Viambajengo katika sentensi  ya Kiswahili huweza kuchopolewa kutoka kiwango cha kirai wakati (Kwkt) na kutua katika kiwango cha Kkijzo. Kutokana na wingi wa  dhima za viambajengo vinavyochopolewa na kutua katika kiwango cha Kkijzo, mbali na virai vya kidesturi vya Kkijzo kazi hii  imependekeza kupanuliwa kwa Kkijzo ili kijumuishe virai vya ziada kama vile: Kirai arifu na Kirai kiwakilishi. Aidha kazi hii, imechunguza  mofosintaksia ya vijalizo changamano ndi- na amba- na kipatanisho kijalizo -o- kama vipashio vinavyotumika kuchopoa viambajengo  katika sentensi za Kiswahili. Lengo hasa la utafiti huu ni kubaini nafasi zinazokaliwa na viambajengo hivi vya uchopoaji kwa mujibu wa  muundo mzima wa sentensi zilizochopolewa. Uchanganuzi wa data katika karatasi hii utafanywa kwa kujikita kwa nadharia ya Kanuni  Finyu hasa mapendekezo ya hivi karibuni ya kigezo cha ugandaji wa kiima.


 


This work examines the syntax of the complement phrase (CP) and its relevance in extraction of elementes in Kiswahili sentences.  Elements in Kiswahili sentences can be extracted from the tense phrase (TP) to various positions within the CP. As a result of the various  elements that land within the CP in a Kiswahili extracted sentence, this paper proposes the expansion of the CP beyond the traditional CP  phrases so as to include additional phrases such as the: Pronoun phrase and Predicate phrase. This work also examines the morphosyntax of the Kiswahili complex complementizers ‘-amba-’ and ‘ndi-’ and the agreement complementiser -o- as elements that  implement complementation in language under study. The aim of this paper is shade light on the positions occupied by these  complementizers in relation to the structure of an extracted Kiswahili sentence. Data analysis is done based on the Minimalist theory  specifically in line with the split CP hypothesis.


Journal Identifiers


eISSN: 2523-0948
print ISSN: 2520-4009