Main Article Content

Taswira ya tanzu za sanaa za maonyesho ya jadi katika tamthilia ya Kiswahili: Mfano wa Mashetani, Pungwa, Ngoma ya Ng’wanamalundina Mashetani Wamerudi


Ezra Nyakundi Mose
Samuel Moseti Obuchi
Mark Mosol Kandagor

Abstract

Makala haya yanachunguza tanzu za sanaa za maonyesho ya jadi na utamaduni wa kiafrika zilizotumiwa kiubunifu na waandishi katika utunzi wa tamthilia ya Kiswahili. Makala yanabainisha tanzu na tamaduni za kiafrika husika katika tamthilia za Mashetani, Pungwa, Ngoma ya Ng’wanamalundi na Mashetani Wamerudi na kufafanua mbinu walizozitumia watunzi katika kusababisha na kuibua maana ya ndani ya kazi zao kupitia kwa ejenzi wa taswira za kimaana. Makala haya vilevile yanashughulikia taswira zinazojengwa na tanzu za sanaa za maonyesho ya jadi na tamaduni za kiafrika zilizotumika katika utunzi wa tamthilia ya Kiswahili. Tamthilia nne za Mashetani, Pungwa, Ngoma ya Ng’wanamalundi na Mashetani Wamerudi zimehakikiwa kwa misingi ya nadhadharia za Uhistoria mpya iliyoasisiwa na Greenblat na na nadharia ya Mwingilianomatini iliyoasisiwa na Julian Kristeva. Tanzu za sanaa za maonyesho ya jadi na tamaduni za kiafrika zilizotumiwa katika utunzi wa tamthilia zetu teule zilibainiswa na kisha tukazihakiki kubaini taswira zinazojengwa kupitia kwa matumizi ya aina hiyo katika kujenga dhamira za mwandishi na umbo zima la tamthilia ya Kiswahili.


Journal Identifiers


eISSN: 2523-0948
print ISSN: 2520-4009