Jarida la Mwanga wa Lugha https://www.ajol.info/index.php/mwl
Mwanga Wa Lugha is an international journal published by Moi University, Kenya. The journal publishes peer reviewed articles on issues related to Kiswahili. The journal mainly accepts papers written Kiswahili; however selected papers written in English are also accepted. The journal publishes well researched papers written in the following thematic areas: linguistics, literature, translation & interpretation, as well as other African languages. Authors are also encouraged to write papers on emerging issues in Kiswahili. language, translation & interpretation and other relevant areas on language and literature. It is published bi-annually (September and April) and has been in existence since 2017.

Aims and Scope

Jarida la Mwanga wa Lugha accepts papers written both in Kiswahili and English. It publishes well researched papers written in the following thematic areas: linguistics, literature, translation & interpretation, as well as other African languages. Authors are also encouraged to write papers on emerging issues in Kiswahili language, translation & interpretation and other relevant areas on language and literature.

You can see the journals own website here
en-US ogechinathan@gmail.com (Prof. Nathan Oyori Ogechi) lkirui@mu.ac.ke (Mr. Leonard Kirui) Tue, 25 Feb 2025 05:42:19 +0000 OJS 3.3.0.11 http://blogs.law.harvard.edu/tech/rss 60 Nafasi ya lugha za kiasili katika mchakato wa kutoa huduma za matibabu: mifano kutoka Tumbatu na Kojani, visiwani Zanzibari https://www.ajol.info/index.php/mwl/article/view/289846
Zanzibar ina jamii ambayo ndani yake muna jamiilugha ndogondogo. Ingawa lugha kuu ya mawasiliano ni Kiswahili, matumizi ya lahaja kama lugha za kijamii yanabainika kwa kiasi kikubwa katika jamiilugha zilizo mahususi. Matumizi ya lugha za kijamii yana mchango mkubwa katika kufanikisha mawasiliano baina ya watu wa jamiilugha. Lengo la makala haya ni kubainisha umuhimu wa lugha za kijamii katika huduma za afya pamoja na athari za kutozingatiwa lugha za kijamii katika huduma za afya, huku mtafiti akirejelea jamiilugha mahususi za Zanzibar. Kwa hiyo, makala yaligundua umuhimu wa lugha za kijamii kama vile elimu ya afya kuwafikia walengwa kwa urahisi, kufanikisha mawasiliano baina ya mtoa huduma na mpokea huduma za afya, n.k. Aidha, makala yanaelezea athari zinazojitokeza katika huduma za afya ambazo chanzo chake ni kutozingatia lugha ya mawasiliano ya jamii husika. Athari hizo ni kama vile woga wa kujieleza kwa upande wa mgonjwa, muuguzaji na hata mtabibu, ambapo huchangia kutopata tiba stahiki, n.k.
Ulfat Abdulaziz Ibrahim, Chuo Kikuu cha Dodoma Copyright (c) 2025 Jarida la Mwanga wa Lugha https://creativecommons.org/licenses/by-nc/4.0 https://www.ajol.info/index.php/mwl/article/view/289846 Tue, 25 Feb 2025 00:00:00 +0000 Usayansi wa miiko ya Waafrika na Uhalisia wake kwa Jamii ya Kileo: mifano kutoka Jamii ya Wapare https://www.ajol.info/index.php/mwl/article/view/289847
Makala haya yanahusu usayansi wa miiko ya Waafrika na uhalisia wake kwa jamii ya kileo. Mifano iliyorejelewa ni ya jamii ya Wapare wa Mwanga mkoani Kilimanjaro. Kutokana na dhima muhimu ya miiko katika ustawi wa jamii kimaadili, makala haya yanakusudia kuweka bayana usayansi wa miiko ya Wapare. Jambo hilo ni muhimu kwa kuwa, linashadidia hoja ya kuwa jamii haiwezi kutenganishwa na miiko kutokana na mwingiliano wa moja kwa moja kati ya jamii na miiko hiyo. Toka jadi, miiko imekuwa na dhima adhimu ya kusimamia maisha ya wanadamu kwa kuendeleza maadili yanayoiwezesha jamii kuishi kwa namna bora. Uzoefu unaonesha kuwa, miiko na jamii ni vitu visivyoweza kutenganishwa. Kwa hali hiyo, jamii isiyo na miiko haipo. Data kwa ajili ya makala haya zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya usaili huru na uchambuzi wa matini. Mbinu hizo ziliwawezesha watafiti kupata taarifa nyingi kuhusu usayansi unaodhihirika kwenye miiko na uhalisia wake. Nadharia ya Taalimu ina Kwao na Fasihi ina Kwao, ndio iliyotumiwa kwenye mwendelezo wa uchunguzi na uchambuzi wa makala haya. Matokeo ya utafiti wa makala haya yalionesha kuwa, miiko ya jamii ina uhalisia kwenye maisha ya jamii ya kileo kutokana na dhima zake. Pia ilibainika kuwa, miiko ina misingi madhubuti ya kisayansi na hivyo kudhihirisha mantiki kuwa, iliwekwa baada ya kufanyiwa tathmini na kuonekana kuwa ni ya muhimu. Kwa hali hiyo, jamii za Kiafrika zinahimizwa kuendeleza miiko yenye manufaa kwa jamii zao ili kuimarisha maisha ya kila siku.
Hatibu Sadi, James Ontieri, Tigiti S. Y. Sengo Copyright (c) 2025 Jarida la Mwanga wa Lugha https://creativecommons.org/licenses/by-nc/4.0 https://www.ajol.info/index.php/mwl/article/view/289847 Tue, 25 Feb 2025 00:00:00 +0000 Mwingilianomatini katika utanzu wa riwaya: mshabaha kati ya Nyuso za Mwanamke na Wenye Meno https://www.ajol.info/index.php/mwl/article/view/289848
Kazi za kifasihi huhusiana, hurejeleana na huingiliana katika mchakato wa kuandikwa kwake, lakini mambo haya hujibainisha kwa uwazi zaidi katika mchakato wa upokezi na ufasiri wa kazi hizo. Bakhtini, mwasisi wa Nadharia ya Mwingilianomatini, anahoji kwamba utanzu wa riwaya una uwezo na wasifu wa kutumia na kushirikisha kiutunzi nduni za tanzu nyingine na bado utanzu huu ukabakia na sifa zake kama utanzu. Kwa mfano, riwaya inaweza kuhusisha na kushirikisha kiutunzi sifa au nduni ya mazungumzo ambayo aghalabu hubainika katika utanzu wa tamthilia au ikahusisha kanuni za ushairi na bado ikabakia kama riwaya. Mnadharia huyu anasema kwamba utanzu wa riwaya una upekee kwa sababu una uwezo wa kuchota sifa, mbinu na mikakati ya kiutunzi ya tanzu nyingine na kuzijumlisha katika kurutubisha muundo na usanifu wake kwa njia anuwai. Sifa hizi za kuhusiana, kurejeleana na kuingiliana kwa nduni za kiutunzi, ni uhalisia unaojitokeza kwa wingi katika tungo za Said Ahmed Mohamed. Kauli hii inahalisi kuhoji kuwa kuna kiasi kikubwa cha mwingilianomatini kinachojitokeza katika kazi za mtunzi huyu. Hali hii inashawishi na kuchochea shauku ya kiutafiti kutaka kubaini kama Said Ahmed anajikariri kiutunzi au kama kuakisika kwa nduni sawia kutoka kazi moja hadi nyingine ni ufundi wa kukuza na kuimarisha mbinu zake za kiutunzi. Hivyo, mchango wa makala hii katika kuziba pengo hilo ni kuchunguza jinsi riwaya mbili za Said Ahmed: Nyuso za Mwanamke (2010) na Wenye Meno (2014) zinavyoingiliana katika vipengele vya maudhui na uhusika. Usampulishaji wa kimakusudi umetumika kuteua kazi hizi. Kwa ujumla, mwelekeo wa makala ni wa mwingilianomatini.
Alex Kinyua , Mwenda Mbatiah, Simon Ongarora Copyright (c) 2025 Jarida la Mwanga wa Lugha https://creativecommons.org/licenses/by-nc/4.0 https://www.ajol.info/index.php/mwl/article/view/289848 Tue, 25 Feb 2025 00:00:00 +0000 Usawiri wa wanawake wenye uwezo katika muziki wa bongo fleva nchini Tanzania https://www.ajol.info/index.php/mwl/article/view/289851
Kwa kutumia mkabala wa ulinganishi, makala haya yanajadili uhusiano wa kijinsia unaobainishwa katika muktadha ambao mwanamke ndiye mmiliki wa mali na ambaye ana fursa katika vyombo vya kufanya maamuzi. Tafiti nyingi zinazungumzia suala la ujinsia zikijikita katika kumwangalia mwanamke kama chombo kinachotumiwa na wanaume katika kutimiza matakwa yao. Pia, zinasawiri namna mwanamke anavyozingirwa na mfumo usio mpa fursa za uhuru binafsi pamoja na maendeleo. Makala haya yanalenga kuleta ukengeushi wa suala hili, kwa kumtazama mwanamke ambaye ana uwezo wa kimaendeleo, mathalani uwezo wa kielimu, kiuchumi, kisiasa, na hata kushiriki katika vyombo vya maamuzi, jinsi ambavyo uhusiano wake ndani ya jamii unavyosawiriwa. Kwa kutumia nyimbo za muziki wa bongo fleva, kama fasihi simulizi pendwa nchini Tanzania, makala yatajadili mahusiano yake na jinsia nyingine na hata na jamii kwa ujumla. Katika makala haya, ulinganishi wa nyimbo za mziki wa bongo fleva zilizoimbwa na jinsia tofauti utafanyika.
Zawadi Daniel Limbe Copyright (c) 2025 Jarida la Mwanga wa Lugha https://creativecommons.org/licenses/by-nc/4.0 https://www.ajol.info/index.php/mwl/article/view/289851 Tue, 25 Feb 2025 00:00:00 +0000 Mitazamo ya waafrika kuhusu urithishwaji wa mali: uchunguzi wa bunilizi za Kiswahili https://www.ajol.info/index.php/mwl/article/view/289853
Kurithisha mali katika jamii nyingi za Kiafrika ni suala linalohifadhi na kuendeleza utamaduni wa jamii. Hivyo, thamani ya mwanadamu katika ulimwengu wake hubainika pia kupitia mali anazorithisha wengine. Vilevile, kupitia mali hizo, mrithishaji anaendelea kuishi katika fikra za wanaorithishwa hata baada ya kifo chake. Kwa msingi huo, urithishwaji wa mali ni hazina inayoendeleza kizazi na kuleta kumbukumbu idumuyo katika ulimwengu halisi wa mwanadamu. Fasihi ni akiso la maisha ya mwanadamu katika mazingira yake halisi. Kwa mantiki hiyo, bunilizi za Kiswahili huhifadhi na kudokeza misingi mbalimbali inayozingatiwa katika kuendesha maisha ya jamii. Mathalani, ile inayohusu suala la urithishwaji wa mali kupitia wahusika wanaosukwa kwa ustadi unaokidhi haja ya kufikisha maudhui lengwa. Hata hivyo, haijaelezwa bayana mitazamo ya Waafrika kuhusu suala la urithishwaji wa mali kwa kuhusianisha na bunilizi za Kiswahili. Hivyo basi, makala hii imeshughulikia jambo hilo kwa kujiegemeza katika riwaya za Rosa Mistika (1971) na Dunia Uwanja wa Fujo (1975). Makala hii ni matokeo ya data zilizopatikana maktabani kwa kutumia mbinu ya usomaji. Vilevile, katika uchunguzi, uchanganuzi na uwasilishaji wa matokeo hayo, misingi ya Nadharia ya Sosholojia ya Kifasihi imetumika. Matokeo yanaonesha kuwa katika suala la urithishwaji wa mali kwa Waafrika, kuna mitazamo mbalimbali inayozingatiwa. Makala hii inajadili mitazamo mikuu mitatu, ambayo ni: mtazamo wa kitamaduni, kihiari, na kimabavu.
Martina Duwe, Adria Fuluge Copyright (c) 2025 Jarida la Mwanga wa Lugha https://creativecommons.org/licenses/by-nc/4.0 https://www.ajol.info/index.php/mwl/article/view/289853 Tue, 25 Feb 2025 00:00:00 +0000 Ukiushi wa taswira dumifu za uana katika ugavi wa kazi na majukumu: tathmini ya hadithi teule za Kiswahili za watoto https://www.ajol.info/index.php/mwl/article/view/289854
Makala hii inachunguza ukiushi wa taswira dumifu za uana katika ugavi wa kazi na majukumu kwenye hadithi za Kiswahili za watoto. Lengo kuu hasa ni kupambanua namna ambavyo ugavi wa kazi na majukumu kwenye hadithi teule za Kiswahili za watoto umekiuka taswira dumifu za uana. Nadharia ya Udenguzi ilitumika kuwa kiunzi cha nadharia na vilevile katika uchanganuzi wa data. Utafiti huu ulizingatia muundo wa kimaelezo na mbinu ya uhakiki makinifu wa matini. Data iliyotumika katika makala hii ilitokana na uhakiki wa hadithi 11 za Kiswahili za watoto. Hadithi zilizochanganuliwa zilisampulishwa kimakusudi kwa kuzingatia malengo ya utafiti. Uwasilishaji wa matokeo ya utafiti ulifanywa kwa kutumia maelezo. Matokeo ya utafiti huu yanadhihirisha kuwa kazi kama vile ualimu, udaktari, uaskari, uanajeshi, urubani, ukulima, uhadhiri, ufanyi biashara, na uhakimu ulifanywa na wahusika wa kike. Aidha, majukumu kama vile kulima, kufyeka, kusukuma toroli, kulisha ng’ombe, na kuchunga mifugo yalifanywa na wahusika wa kike huku wahusika wa kiume wakitekeleza majukumu kama vile kuosha vyombo na kuandika meza. Kwa kuhitimisha, matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kuwa taswira dumifu za uana zimekiukwa katika ugavi wa kazi na majukumu, kwenye hadithi za Kiswahili za watoto. Makala hii hivyo basi inapendekeza matibaa, mashirika ya kuchapisha vitabu vya watoto na asasi za kiserikali zibuni sera na miongozo itakayohakikisha kuwa taswira dumifu za uana zinadhibitiwa hususan katika ugavi wa kazi na majukumu. Mwisho, makala hii pia imedhihirisha kuwa fasihi ya Kiswahili ya watoto ni nyenzo muhimu katika Jitihada za utatuzi wa migogoro ya kiuana ambayo huathiri mahusiano ya kijinsia katika jamii.
Simon Ekiru, Mosol Kandagor, Magdaline Wafula Copyright (c) 2025 Jarida la Mwanga wa Lugha https://creativecommons.org/licenses/by-nc/4.0 https://www.ajol.info/index.php/mwl/article/view/289854 Tue, 25 Feb 2025 00:00:00 +0000 Uamili wa ngazi ya utambuzi katika riwaya za Kiswahili https://www.ajol.info/index.php/mwl/article/view/289870
Makala haya yanaangazia na kuchunguza dhana ya ngazi ya utambuzi na uamili wake katika riwaya za Kiswahili zilizoteuliwa makusudi kuukita na kuuendeleza mjadala unaodhamiriwa katika makala haya. Ngazi ya utambuzi ni mojawapo ya ngazi mbalimbali za ufokasi zilizopendekezwa na wananaratolojia kama vile Uspensky (1973) na Rimmon-Kenan (1983). Kimsingi, ufokasi ni mtazamo ambao huchukuliwa katika kuwasilisha simulizi na kuikuza hadithi tawala kwa ujumla. Ufokasi unajishughulisha kubaini ni nani anayeona kinachosimuliwa katika simulizi. Ufokasi ni istilahi iliyobuniwa na wananadharia ya naratolojia kurejelea kile ambacho katika uhakiki wa kijadi kilijulikana kama kitazamio. Abrams (1993) anaifafanua dhana hii ya ufokasi kuwa inarejelea jinsi hadithi inavyowasilishwa yaani, njia ambazo mwandishi anazitumia kusawiri na kuwasilisha kwa msomaji wahusika, dayalojia, matendo, mandhari na matukio yanayounda simulizi katika kazi ya bunilizi. Kwa upande wake, Hawthorn (2010:122) anasema kwamba, istilahi ya “kitazamio” haipambanui ni nani msemaji na nani anayeona na nini anachoona katika simulizi. Hii ndiyo sababu Genette (1972) alibuni istilahi hii ya ufokasi kama mkakati wa kuwezesha kutambua na kutofautisha kati ya msemaji na mfokasi katika simulizi za kifasihi. Kwa kujikita katika dhana hii ya ufokasi, msomaji au mchanganuzi anaweza kutambua pale ambapo mwandishi ndiye aliyeyashuhudia au anayeyashuhudia matukio au pale ambapo mwandishi anamtumia mmojawapo wa wahusika kuwasilisha ujumbe wake. Ili kutuwezesha kubainisha uamili wa ngazi ya utambuzi katika riwaya ya Kiswahili, data ya kuudhibiti na kuthibitisha madai ya mjadala tawala itatolewa katika riwaya za Kiswahili zilizoteuliwa makusudi zikijumuisha (C.S.L. Chachage, 2005), Nyuso za Mwanamke (S.A. Mohamed, 2010), Harufu ya Mapera (K. W. Wamitila, 2012), Hujafa Hujaumbika (F.M. Kagwa, 2018), Haini (Adam Shafi, 2002), na Ndoto ya Almasi (Ken Walibora, 2006). Uteuzi wa riwaya hizi unahalalishwa kwa misingi kwamba, hizi ni riwaya zilizo na matini pana zinazowezesha udondoaji wa mifano faafu inayodhihirisha ngazi za ufokasi na wakati huo huo kudhihirisha uamili wa ngazi hizo katika simulizi. Mjadala wa kimsingi katika makala haya umekitwa na kuongozwa na madai ya teneti za kimsingi za Nadharia ya Naratolojia ambayo inatambua ufokasi na uhusika kama vipengele muhimu katika uwasilishaji wa simulizi.
Dinah Sungu Osango, Mwenda Mbatiah, Rayya Timammy Copyright (c) 2025 Jarida la Mwanga wa Lugha https://creativecommons.org/licenses/by-nc/4.0 https://www.ajol.info/index.php/mwl/article/view/289870 Tue, 25 Feb 2025 00:00:00 +0000 Sababu za mkengeuko wa malezi kwa wahusika katika riwaya ya Rosa Mistika https://www.ajol.info/index.php/mwl/article/view/289871
Ingawa wahusika hukengeuka malezi, wataalamu na wachambuzi hutofautiana katika kuelezea jambo hili. Wapo wanaoona kuwa, kukiuka malezi kwa wahusika katika kazi za fasihi kunasababishwa na wazazi au walezi (Wanjala, 2015; Mbatiah, 2016; Doepke na Zilibotti, 2019). Kwa upande mwingine, wapo wataalamu wanaowatupia lawama watoto kuwa wanabadilika hasa wanapotoka mikononi mwa wazazi na kuingia katika jamii kutokana na kushindwa au kupuuza malezi na maelekezo kutoka kwa wazazi au walezi wao (Ondieki, 2015; Jonas, 2017). Aidha, upande mwingine jamii hulaumiwa kwa kushindwa kuendeleza malezi yanayofaa kutoka kwa wazazi au walezi wa watoto (Mitchell, 2010; Martin, 2017; Sanga, 2018). Tofauti hizi za kimtazamo ndizo zilizosukuma kuandikwa kwa makala hii. Kwa hivyo, makala hii inakusudia kujadili sababu za mkengeuko wa malezi kwa wahusika kwa kutumia riwaya ya Rosa Mistika (Kezilahabi, 1971).
Selestino Helman Msigala Copyright (c) 2025 Jarida la Mwanga wa Lugha https://creativecommons.org/licenses/by-nc/4.0 https://www.ajol.info/index.php/mwl/article/view/289871 Tue, 25 Feb 2025 00:00:00 +0000 Kapitalosenia kama pantoni ya anthroposenia katika riwaya ya Kiswahili: Mfano wa Vipuli vya Figo, Mafuta na Walenisi https://www.ajol.info/index.php/mwl/article/view/289872
Makala haya yanashughulikia kapitalosenia kama pantoni ya anthroposenia katika nchi za Afrika katika riwaya ya Emmanuel Mbogo: Vipuli vya Figo; na za Katama Mkangi: Mafuta na Walenisi. Riwaya hizi tatu zilisomwa na mtafiti na hatimaye data iliyodhihirisha kapitalosenia kama pantoni ya anthroposenia ilitongolewa mintarafu ya lengo la makala haya. Kusudi kuu la makala haya lilikuwa kujadili namna kapitalosenia huvusha anthroposenia kutoka mataifa ya ughaibuni hadi barani Afrika katika riwaya nne teule za Kiswahili katika misingi ya kiuhakikimazingira. Baadhi ya nguzo kuu za nadharia ya uhakikimazingira, kama vile; uongozi mbaya, kifo na uwezo, utamaduni na mazingira, na utandawazi, ziliongoza uhakiki wa makala haya, mintarafu ya lengo la makala. Sababu kuu ya kuhakiki riwaya hizi ilikuwa kukidhia data ya tahakiki zinazohusu mchango wa kapitalosenia katika anthroposenia barani Afrika katika riwaya ya Kiswahili. Ilidhihirika kwamba, kando na mataifa yenye uwezo kuyanyonya yale fukara ya Afrika rasilimali asilia, taaluma, wataalamu, na watumwa kama wafanyakazi madhubuti, yanapujua mazingira ya Afrika bure na kwa hiari yao wenyewe. Ingawa unajisi huu wa kimazingira unaathiri utamaduni na jamii kwa jumla, chumi za Afrika zilidhihirisha udhoofu wa hali ya juu kutokana na kiwango cha ufukara unaokita mizizi katika nchi za Afrika.
Antony Kago Waithiru, Wendo K. Nabea, Sheila P. Simwa Copyright (c) 2025 Jarida la Mwanga wa Lugha https://creativecommons.org/licenses/by-nc/4.0 https://www.ajol.info/index.php/mwl/article/view/289872 Tue, 25 Feb 2025 00:00:00 +0000 Itikadi za ujinsia katika maumbo ya majina ya Kikuria https://www.ajol.info/index.php/mwl/article/view/289873
Majina ni vipengele vya lugha ambavyo hutaja mtu, kitu, hali, mahali, dhana na tendo na huweza kufunua itikadi na matukio katika maisha ya wanajamii. Itikadi ni mawazo ambayo humwongoza kila mtu ulimwenguni katika kutenda anayotenda na hivyo kuhalalisha au kuharamisha matendo anayoyafanya. Makala haya yanajikita katika kuchanganua jinsi maumbo ya majina ya Kikuria katika jamii ya Wakuria iliyoko nchini Kenya hushamirisha itikadi za ujinsia. Itikadi za ujinsia ni imani, mielekeo na mitazamo inayoongoza jamii kuhusu mgawanyo wa majukumu kwa kuangalia jinsia. Lengo kuu la makala haya ni kuainisha jinsi maumbo ya majina ya Kikuria hudumisha na kuendeleza itikadi za ujinsia. Data iliyotumika katika makala haya ilikusanywa kwa njia ya mahojiano ya ana kwa ana na majadiliano ya makundi. Ukusanyaji na uchanganuzi wa data uliongozwa na Nadharia ya Onomastiki. Nadharia hii imekuwa dira katika kubainisha maumbo ya majina ya Wakuria na jinsi maumbo haya huakisi itikadi za ujinsia katika jamii ya Wakuria. Utafiti wetu uliweza kubainisha kuwa vipo vipashio ambavyo hudokeza jinsia na shughuli inayohusishwa nazo au nafasi yake katika jamii. Kwa misingi hii, utafiti wetu ulibainisha kuwa jinsia ya kiume kwa mujibu wa majina yao yaliyoteuliwa kiitikadi, ilitengewa shughuli na nafasi zilizoikweza ikilinganishwa na jinsia ya kike.
Roseline Kasuma, James Ogola, Sangai Mohochi Copyright (c) 2025 Jarida la Mwanga wa Lugha https://creativecommons.org/licenses/by-nc/4.0 https://www.ajol.info/index.php/mwl/article/view/289873 Tue, 25 Feb 2025 00:00:00 +0000 ‘Cooking’ masculinity in the digital world: a look at @Amerix’s #MasculitySaturday https://www.ajol.info/index.php/mwl/article/view/289874
Through technology, the digital world has birthed a new space where people can connect with each other. This space has resulted in a shift where concepts are no longer static but constantly shifting. One of these concepts is masculinity. A social construct, the concept of what constitutes masculinity continues to shift as the digital world moves towards both diversity and inclusivity. This paper seeks to explore how a medical consultant, Eric Amunga, has appropriated the digital space to make commentary on various social aspects. Using his X (formerly Twitter) handle @amerix, Amunga runs #MasculinitySaturday, whose ‘teachings’ range from health, relationships, sex to parenting, all in a bid to ‘equip’ men with means with which to navigate manhood. With a following of over 1.2 million followers, this article argues that Amunga has not only created a platform for his ‘teachings’ but also an avenue for the world to engage. Through the ‘replies’ section, members are allowed to comment on the topical issues thus engaging in debate. I thus examine the aesthetics of this discourses and demonstrate how Amunga draws in, engage and sustains his following through New Media and how this relates to the postcolonial experience of the contemporary period in East Africa.
Maina T. Sammy Copyright (c) 2025 Jarida la Mwanga wa Lugha https://creativecommons.org/licenses/by-nc/4.0 https://www.ajol.info/index.php/mwl/article/view/289874 Tue, 25 Feb 2025 00:00:00 +0000 Nafasi ya nyimbo za kizazi kipya katika kufundishia masuala mtambuko katika Mtaala wa Umilisi https://www.ajol.info/index.php/mwl/article/view/289875
Hitaji mojawapo katika Mtaala wa Umilisi nchini Kenya ni kuwa wanafunzi wanapaswa kufundishwa masuala mtambuko. Lengo la kuwafundisha masuala mtambuko ni kuwasaidia wawe wabunifu na wapate ujuzi wa kukabiliana na masuala haya katika mazingira yao ya kila siku. Mtaala huu unasisitiza kuwa mwalimu anapaswa kuwa mbunifu katika ufundishaji wake ili kukuza umilisi wa wanafunzi. Njia mojawapo ya kufundisha masuala kiubunifu ni kupitia matumizi ya nyimbo za kizazi kipya ambazo zina maudhui ya masuala mtambuko mbalimbali. Nyimbo hizi zinapendwa na vijana ambao hujihusisha nazo na wao huzisikiliza kupitia vyombo mbalimbali vya habari. Makala haya yanachanganua baadhi ya nyimbo za kizazi kipya na jinsi mwalimu anavyoweza kuzitumia kufundishia masuala mtambuko darasani ili kufikia malengo yake na matarajio ya jamii kwa ujumla. Nadharia iliyoongoza makala haya ni Nadharia ya Utekelezaji wa Mtaala iliyoasisiwa na Gross (1971).
Lena K. Nyandwaro , Alfred Malugu Copyright (c) 2025 Jarida la Mwanga wa Lugha https://creativecommons.org/licenses/by-nc/4.0 https://www.ajol.info/index.php/mwl/article/view/289875 Tue, 25 Feb 2025 00:00:00 +0000 Challenges of translating conversational implicatures from English to Kiswahili using computer assisted tools: a case of Google Translate https://www.ajol.info/index.php/mwl/article/view/289876
In this study, we investigated challenges faced by computer assisted translation software with special focus on Google Translate, in translating conversational implicatures from English to Kiswahili. The data for this study were sourced from William Shakespeare's play, “The Tragedy of Othello the Moor of Venice” which has been translated to Kiswahili as “Othello, Tanzia ya Mtu Mweusi.” The data was informed by Grice’s (1975) conversational implicature theory, and the relevance-theoretic translation approach as postulated by Gutt (1991). To evaluate the quality of Google Translate computer assisted translation system, we made a comparison of the computer translated output with the human translated text to ascertain to what extent the meaning of the conversational implicatures in the source language is preserved in the target text. We further examined challenges encountered by Google Translate in the process of translating conversational implicatures and suggested what could be done to improve Google Translate method to ensure accuracy in translating conversational implicatures. The results indicate that, there is inferior translation quality of the target text with ambiguous words and sentences. Also, it was observed that it is challenging to translate conversational implicatures using Google Translate because it has not been programmed to process aspects of source culture or adapt to the aspects of target culture thus cannot correctly translate conversational implicatures. Besides that, other challenges posed range from lexical, syntactic, and semantic to pragmatic mismatch.
Lilian Chacha, Iribe Mwangi Copyright (c) 2025 Jarida la Mwanga wa Lugha https://creativecommons.org/licenses/by-nc/4.0 https://www.ajol.info/index.php/mwl/article/view/289876 Tue, 25 Feb 2025 00:00:00 +0000 Lugha na muktadha wa matumizi yake katika sekta ya kilimo nchini Tanzania https://www.ajol.info/index.php/mwl/article/view/289877
Mlolongo wa nyaraka za serikali, matamko na kauli za wanasiasa zinataja baadhi tu ya maeneo mahususi ya matumizi ya lugha Nchini Tanzania. Miongozo hiyo inaonekana kusisitiza zaidi hasa matumizi ya lugha katika mfumo wa elimu na mafunzo. Maeneo mengine ya utoaji wa huduma za jamii ikiwamo kilimo hayajapata kutolewa maelekezo kuhusu matumizi ya lugha. Matokeo yake ni vigumu kufahamu lugha gani inatumika katika muktadha upi wa utoaji wa huduma za kilimo. Hivyo, utafiti huu umechunguza lugha zinazotumika na muktadha wa matumizi yake katika sekta ya kilimo mkoani Morogoro nchini Tanzania. Kwa kutumia mbinu za hojaji, usaili na uchambuzi wa nyaraka, data zilikusanywa kutoka kwa wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo na katika matini za utoaji wa huduma za kilimo. Uchambuzi wa data umeongozwa na Nadharia ya Ufanyaji Uamuzi ya Eastman (1983). Matokeo ya utafiti huu yanadhihirisha kwamba sekta ya kilimo inatawaliwa na hali ya wingilugha. Lugha zilizobainika kutumiwa katika utoaji wa huduma za kilimo ni Kiswahili, Kiingereza, Kifaransa, Kihispaniola, Kiluguru, Kipogoro, Kikagulu, Kinguu, na Kisagara. Hata hivyo, uwiano wa matumizi ya lugha hizo unatofautiana. Zipo lugha zinazotumika kwa kiwango cha juu na zingine kwa kiwango cha chini. Katika muktadha wa mashamba darasa lugha ya Kiswahili inatawala ilhali katika muktadha wa maduka ya pembejeo za kilimo na mfumo wa elimu na mafunzo, Kiingereza ndicho kinachotawala. Kwa hiyo, utafiti huu umehitimisha kuwa kuna haja ya kuwa na sera itakayoongoza matumizi ya lugha katika utoaji wa huduma za kilimo nchini Tanzania.
Peter Masanja Copyright (c) 2025 Jarida la Mwanga wa Lugha https://creativecommons.org/licenses/by-nc/4.0 https://www.ajol.info/index.php/mwl/article/view/289877 Tue, 25 Feb 2025 00:00:00 +0000 Ujitokezaji wa viambishi vya nafsi katika Kiarabu, Kitumbatu na Kiswahili https://www.ajol.info/index.php/mwl/article/view/289878
Makala haya yanalenga kuchunguza ujitokezaji wa viambishi vya nafsi katika Kiarabu Kitumbatu na kuvilinganisha na Kiswahili. Lengo la uchunguzi huo ni kutaka kubaini jinsi vipengele hivyo vinavyoingiliana na kusigana. Hii inatokana na ukweli kwamba mapisi ya lugha ya Kiswahili na lahaja zake pamoja na lugha ya Kiarabu mpaka sasa hayajatindimaa kwa kuwa lugha hizi zilikuwa na mtagusano na muasala wa muda mrefu tangu 800 BK. Kutokana na hali hiyo, kumeibuka mitazamo kinzani juu ya uhusiano wa Kiswahili na Kiarabu. Kuwapo kwa baadhi ya maneno ya Kiarabu katika Kiswahili kumechochea hoja kwamba Kiswahili kinatokana na Kiarabu. Mjadala huo ni wa muda mrefu ambao unaendelea hadi sasa. Baadhi ya tafiti tangulizi zimebainisha idadi kubwa ya maneno ya Kiswahili yenye asili ya Kiarabu. Hata hivyo, mfanano huo wa kimsamiati baina ya Kiswahili na Kiarabu haujitoshelezi kutoa hitimisho juu ya chimbuko la Kiswahili. Baadhi ya watafiti waliochunguza maneno ya Kiarabu katika Kiswahili wamebaini kuwapo kwa asilimia kubwa ya mfanano wa kategoria ya nomino baina ya lugha hizi mbili kuliko katika kategoria zingine. Hivyo, pamoja na kuwapo kwa kategoria mbalimbali za maneno, utafiti huu umejibana kushughulikia jinsi viambishi vya nafsi vinavyojitokeza katika kategoria ya vitenzi vya Kiarabu, Kitumbatu na kuvilinganisha na Kiswahili. Hii ni kwa sababu kwa kuwa imeshatibitika kwamba, Kitumbatu ni miongoni mwa lahaja ya Kiswahili, ujitokezaji huo wa viambishi utatupa mwanga kati ya uhusiano wa Kiarabu na Kiswahili. Chanzo cha data za utafiti huu zimekusanywa kupitia usomaji wa nyaraka, vitabu na kamusi mbalimbali zilizoandikwa kuhusu kategoria hiyo. Vilevile, tulipitia nyaraka hizo ili kupata maarifa ya jumla kuhusu ujitokezaji wa viambishi vya nafsi kwa mujibu wa waandishi mbalimbali. Data zingine zilikusanywa uwandani kupitia mbinu ya usaili na hojaji kwa wazungumzaji wa Kiarabu na Kitumbatu. Aidha, utafiti huu umeongozwa na Nadharia ya Fonolojia Umbo Upeo kuanzia sasa (UU). Kwa ujumla matokeo ya utafiti huu yameonesha kwamba Kitumbatu kina uhusiano zaidi na Kiswahili kuliko Kiarabu. Hii ni kudhihirisha kwamba Kiswahili na Kiarabu ni lugha mbili ambazo hazina uhusiano wa kimnasaba kwa kuwa hazikuchipukia kutoka kwenye lugha yenye asili moja.
Sauda Uba Juma Copyright (c) 2025 Jarida la Mwanga wa Lugha https://creativecommons.org/licenses/by-nc/4.0 https://www.ajol.info/index.php/mwl/article/view/289878 Tue, 25 Feb 2025 00:00:00 +0000 Mabadiliko ya utabaka: ulinganishi wa riwaya za Kuli na Pendo la Karaha https://www.ajol.info/index.php/mwl/article/view/289879
Utabaka hudhihirika katika jamii ya kibepari ambayo hugawanya watu kulingana na uwezo wao wa kumiliki na kudhibiti njia za uzalishaji mali. Marx anadai kuwa, historia ya jamii ndiyo historia ya mgogoro wa matabaka. Kutawaliwa kwa watu wa tabaka la chini na wale wa juu kunaeleza jumla ya muundo wa jamii. Jamii ina tabia ya kubadilika kadri ya mpito wa wakati. Kutokana na sifa hii, makala hii itachunguza mabadiliko ya utabaka katika jamii ya kibepari kwa kulinganisha matukio ya kitabaka katika riwaya za Kuli (Shafi, 1979) na Pendo la Karaha (Habwe, 2014). Riwaya hizi zimeandikwa katika vipindi tofauti, Kuli imeandikwa katika karne ya 20 na Pendo la Karaha katika karne ya 21. Kwa hivyo, tunatarajia kuwa zitakidhi haja yetu ya kulinganisha ili kubaini ikiwa kuna mabadiliko yaliyokumba utabaka. Tunaamini kuwa utabaka ungalipo lakini kuna vipengele ndani yake vilivyobadilika kutokana na mpito wa wakati. Tutaongozwa na Nadharia ya Umarx iliyoasisiwa na Karl Marx na Friedrich Engels. Nadharia hii huonyesha migogoro ya kitabaka iliyopo katika jamii ambapo watu wa tabaka la chini hunyanyaswa na wale wa tabaka la juu. Tunatarajia kuwa utafiti huu utachangia katika fasihi ya Kiswahili na kuwa na umuhimu kwa wasomi katika viwango mbalimbali vya elimu na jamii kwa jumla.
Virginia Wambui Mwathi, Vifu Makoti, John Mutua Copyright (c) 2025 Jarida la Mwanga wa Lugha https://creativecommons.org/licenses/by-nc/4.0 https://www.ajol.info/index.php/mwl/article/view/289879 Tue, 25 Feb 2025 00:00:00 +0000 Changamoto za kuingiza antonimu katika kamusi wahidiya za Kiswahili: Mifano kutoka Kamusi Kuu ya Kiswahili Toleo la Tatu (KKK3) https://www.ajol.info/index.php/mwl/article/view/289895
Makala haya yamechunguza changamoto za kuingiza antonimu katika fasili za vidahizo vya kamusi wahidiya za Kiswahili. Data zilikusanywa maktabani kwa njia ya usomaji matini. Matini iliyosomwa kwa ajili ya mifano ni Kamusi Kuu ya Kiswahili Toleo la Tatu (KKK3). Vidahizo 379 kati ya 22675 vya KKK3 vilibainika kuwa vimetumia antonimu kufafanua maana zake. Vidahizo vilivyokusanywa vilitumika kama data kushadidia hoja. Data hizo zimechanganuliwa kwa kutumia mikabala ya kitaamuli na kitakwimu. Aidha, Nadharia Jumuishi ya Leksikografia aliyoiasisi Herbert Wiegand imeongoza uchanganuzi wa data. Nadharia hii imeegemea kwenye misingi inayohusu kujali mahitaji ya walengwa wa kamusi, matumizi ya maarifa ya nadharia nyingine nje ya leksikografia na kuangalia kamusi kwa kuzingatia kanuni asilia za wanaleksikografia tangulizi. Makala yamebainisha changamoto za antonimu kileksikografia. Mosi, ni kubadilika kwa kategoria ya kidahizo na antonimu. Pili, ni ukosefu wa urari wa idadi ya antonimu ndani ya kitomeo. Tatu, ni ukosefu wa urari wa mpangilio wa antonimu ndani ya vitomeo. Nne, ni kutozingatia alama za uakifishi. Tano, ni kuwapo kwa upendeleo wa kileksikografia. Sita, ni mpishano wa kidhana kati ya kidahizo na ufafanuzi wake unaohusu antonimu. Makala yanapendekeza watungaji wa kamusi wazingatie kanuni za kufafanua vidahizo vya kiantonimu kwa namna isiyomsumbua mlengwa wa KKK3 kuzing’amua maana zilizokusudiwa kumfikia.
Jeremiah Swallo Andrew, Musa M. Hans Copyright (c) 2025 Jarida la Mwanga wa Lugha https://creativecommons.org/licenses/by-nc/4.0 https://www.ajol.info/index.php/mwl/article/view/289895 Tue, 25 Feb 2025 00:00:00 +0000 Mchango wa uhakiki-maeneo katika ufasiri wa ploti katika hadithi fupi ya Kiswahili https://www.ajol.info/index.php/mwl/article/view/289899
Utafiti wetu umejikita katika kuhusisha ufasiri wa ploti katika hadithi fupi ya Kiswahili na maeneo ya kijiografia kama yalivyosawiriwa katika hadithi fupi zenyewe. Nadharia mwafaka inayoshughulikia maeneo ya kijiografia katika kazi za kibunilizi ni uhakiki-maeneo. Kupitia usampuli maksudi tuliteua hadithi ya “Ahadi ya Mwana” ya Aidah Mutenyo kutoka diwani ya Safari ya Matarajio na hadithi Nyingine. Matokeo ya uchunguzi wetu yamedhibitisha kuwa uhakiki-maeneo wa maeneo ya kijiografia katika hadithi fupi ya Kiswahili, una manufaa makubwa kwa msomaji wa hadithi fupi ya Kiswahili kwa kuwa ubanifu wa maelezo kuhusu maeneo yenyewe huenda ukasababisha hadithi fupi kutofasirika kwa wepesi na haraka.
J. M. Shitemi , T. Olali , E. M. Mbuthia , A. Wanjala Copyright (c) 2025 Jarida la Mwanga wa Lugha https://creativecommons.org/licenses/by-nc/4.0 https://www.ajol.info/index.php/mwl/article/view/289899 Tue, 25 Feb 2025 00:00:00 +0000