Main Article Content

Nafasi ya lugha za kiasili katika mchakato wa kutoa huduma za matibabu: mifano kutoka Tumbatu na Kojani, visiwani Zanzibari


Ulfat Abdulaziz Ibrahim
Chuo Kikuu cha Dodoma

Abstract

Zanzibar ina jamii ambayo ndani yake muna jamiilugha ndogondogo. Ingawa lugha kuu ya mawasiliano ni Kiswahili, matumizi ya lahaja kama lugha za kijamii yanabainika kwa kiasi kikubwa katika jamiilugha zilizo mahususi. Matumizi ya lugha za kijamii yana mchango mkubwa katika kufanikisha mawasiliano baina ya watu wa jamiilugha. Lengo la makala haya ni kubainisha umuhimu wa lugha za kijamii katika huduma za afya pamoja na athari za kutozingatiwa lugha za kijamii katika huduma za afya, huku mtafiti akirejelea jamiilugha mahususi za Zanzibar. Kwa hiyo, makala yaligundua umuhimu wa lugha za kijamii kama vile elimu ya afya kuwafikia walengwa kwa urahisi, kufanikisha mawasiliano baina ya mtoa huduma na mpokea huduma za afya, n.k. Aidha, makala yanaelezea athari zinazojitokeza katika huduma za afya ambazo chanzo chake ni kutozingatia lugha ya mawasiliano ya jamii husika. Athari hizo ni kama vile woga wa kujieleza kwa upande wa mgonjwa, muuguzaji na hata mtabibu, ambapo huchangia kutopata tiba stahiki, n.k.


Journal Identifiers


eISSN: 2709-8419
print ISSN: 2412-6993