Main Article Content
Uchanganuzi wa Tungo zenye Upinduzi wa Kimahali katika Lugha ya Kiswahili: Sifa za Muundo wa Taarifa na Sababu za Upinduzi wa Kimahali katika Mawasiliano
Abstract
Kuna uhusiano baina ya udarajia wa dhima za kisemantiki na dhima za kisarufi. Uhusiano uliopo ni kwamba kiambajengo kilichopo katika nafasi ya juu katika udarajia huo ndicho kinapaswa kuwa kiima na sio kiambajengo kilichopo katika nafsi ya chini. Tungo zenye upinduzi wa kimahali zinakiuka uhusiano huo. Katika tungo hizo, kimahali, ambacho kipo katika nafasi ya chini, kinakuwa kiima ilihali sio mtenda au kithimu. Wataalamu mbalimbali wamefafanua tungo hizi katika lugha za Kibantu. Licha ya kufanya hivyo, hakuna uwazi kuhusu sifa za muundo wa taarifa na sababu za upinduzi wa kimahali katika mawasiliano. Hivyo, makala haya yanafafanua na kubainisha masuala hayo katika lugha ya Kiswahili. Data zilizotumika zimepatikana kwa mbinu ya uchambuzi wa matini, upimaji wa usahihi wa kisarufi pamoja na usaili. Data hizo zimefasiriwa kwa kutumia misingi ya Nadharia ya Sarufi Leksia Amilifu (Bresnan na Kaplan, 1982). Baada ya kufasiri data hizo, makala haya yanabainisha kwamba muundo wa taarifa wa tungo hizi una aina mbili za taarifa, yaani mada na fokasi. Aidha, makala yanafafanua kwamba upinduzi wa kimahali unatokea kwa sababu ya umadaishaji wa kimahali na ufokalishaji wa kithimu/mtenda.