Main Article Content

Nafasi ya nyimbo katika ufundishaji wa msamiati wa Kiswahili kwa watoto wa elimu ya awali


Tumaini Samweli Mugaya

Abstract

Lengo kuu la makala haya ni kuonesha nafasi ya nyimbo katika ufundishaji wa msamiati wa lugha ya Kiswahili miongoni mwa watoto wa elimu ya awali. Utafiti huu umeonesha kupandikiza hali mpya ya matumizi chanya ya nyimbo kwa walimu na watoto katika utoaji na upokeaji wa elimu. Mkabala wa kitaamuli umetumika kubainisha data katika mada ndogondogo. Usampulishaji lengwa ulitumika kuwapata watoataarifa 20. Nadharia ya Vygotsky ya Ujenzi wa Jamii imetumika kuonesha kuwa nyimbo na msamiati wa lugha ni tendo la kijamii katika kutolea maarifa. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba kuna uhusiano mkubwa baina ya nyimbo na ufundishaji wa msamiati wa lugha. Imebainika kuwa nyimbo ni njia muhimu ya mawasiliano miongoni mwa wanajamii. Njia hii hutumika katika miktadha mbalimbali ikiwa na dhima ya kuburudisha au kufikisha ujumbe fulani katika jamii. Hii ni njia nyepesi na rahisi zaidi kwa watu hususani watoto kwani nyimbo huwashirikisha pamoja kupata uelewa wa msamiati na kile mtoto anachofundishwa kupitia uimbaji. Hivyo basi, nyimbo zina nafasi kubwa katika ufundishaji na ujifunzaji wa msamiati katika kuijenga lugha ya Kiswahili na kuendeleza maarifa ya watoto. Aidha, nyimbo huleta motisha na huwajenga watoto kiakili, kihisia, kimwili na kijamii katika kutafsiri maisha yao ya baadaye.


Journal Identifiers


eISSN: 2546-2202
print ISSN: 0856-0129