Main Article Content

Mfumo Faafu wa Ukonganyaji Istilahi za Sayansi na Teknolojia katika Kiswahili


Zabron T. Philipo

Abstract

Makala haya ya naonesha mfumo faafu wa ukonganyaji I stilahi za Sayansi na Teknolojia (kuanzia sasa IST) katika Kisw ahili . Uundaji wa istilahi  hususani katika lugha ya Kiswahili umeonekana kutilia mkazo zaidi katika mtazamo wa ukonganyaji istilahi mahususi. Mtazamo unaosisitiza  ukusanyaji istilahi kwa ajili ya uundaji istilahi kutokana na mwitikio wa wanaistilahi kutaka kuunda istilahi mpya. Pia, ukonganyaji huu ni ule wa  kuandaa kongoo ya istilahi kwa ajili uundaji istilahi. Hoja na mifano zilikusanywa kutokana na usomaji wa nyaraka hususani, nyaraka za BAKITA  (Istilahi za Kiswahili) na TATAKI (Kamusi Sanifu Biolojia Fi zikia na Kemia) na usaili. Hoja na mifano hiyo zinahalalisha umakinikiaji wa ukonganyaji  istilahi katika l ugha ya Kiswahili. Makala h aya ya najikita katika mtazamo wa ukonganyaji istilahi tarakibishi . Mtazamo una o sisitiza kanuni tatu za  kuzingatia; mosi, ukusanyaji istilahi wa kongoo; pili, ukusanyaji wa kanzidata ya istilahi na taarifa husianifu yaani, kwa lengo la kuanzisha benki ya  istilahi a u utunzi wa kamusi ya istilahi za kiufundi; na tatu, ukusanyaji istilahi wa uendelezaji stahilifu. Lengo la ukongan yaji istilahi kwa mkabala  huu ni kuwa na uundaji wa istilahi unaokidhi haja ya mawasiliano mahsusi katika nyanja husika. Hivyo, ukonganyaji huu utarekebisha ukonganyaji  uliopo sasa na kuwa na mfumo bora wa ukonganyaji istilahi za fani mbalimbali katika lugha ya Kiswahili. 


Journal Identifiers


eISSN: 2546-2202
print ISSN: 0856-0129