Main Article Content

Matumizi ya Mbinu ya Usimulizi katika Kuibua Dhamira ya Ukombozi wa Kisiasa Kusini mwa Afrika: Uchunguzi wa Nyimbo Teule za Muziki wa Dansi nchini Tanzania 1940-1990


Elizabeth Mahenge

Abstract

Makala haya yanakusudia kuchunguza jinsi mbinu ya usimulizi ilivyotumika katika kuwasilisha dhamira ya ukombozi kwenye nyimbo teule za muziki wa dansi nchini Tanzania. Kimsingi, muziki wa dansi ulivuma sana kipindi cha miaka ya 1940-1960. Hiki ni kipindi ambacho kinahusiana moja kwa moja na vuguvugu la masuala ya ukombozi wa bara la Afrika. Kwa kuzingatia muktadha huu, makala haya ni muhimu kwa kuwa muziki uliochunguzwa umesheheni mambo mengi yenye mafunzo mengi kwa dunia yetu ya leo. Kimuundo, makala haya yamegawanyika katika sehemu kuu sita: utangulizi, historia fupi ya muziki wa dansi, methodolojia, nadharia iliyotumika, mjadala na matokeo ya utafiti, na mwisho ni hitimisho.


Journal Identifiers


eISSN: 2546-2202
print ISSN: 0856-0129