Main Article Content

Thamani ya Ujumi wa Kiafrika katika Hadithi Fupi Simulizi za Kiswahili


Aginiwe Nelson Sanga

Abstract

Kuibuka kwa mijadala kuhusu ujumi wa Kiafrika katika nyuga mbalimbali ukiwamo uga wa fasihi, kumechangiwa na mahusiano ya kihistoria ya Waafrika na watu wa mataifa mengine, hususani watu kutoka jamii za Kimagharibi. Kwa karne nyingi Waafrika wameonekana ni jamii ya watu duni, washenzi, washirikina na kwamba Afrika hakuna chochote chenye maana wala chenye kuvutia (Neugebauer, 1991). Mitazamo ya namna hiyo katika kutathmini ulimwengu wa Kiafrika haijaishia kwa wageni tu, bali hata baadhi ya Waafrika walioathiriwa na elimu ya Kimagharibi huuzungumzia utamaduni wa Kiafrika na fasihi yake kwa namna hiyohiyo. Hili linadhihirika bayana pale tunapoona fasihi simulizi ya Kiafrika ikiwamo fasihi simulizi ya Kiswahili inapigwa kumbo na Waafrika wenyewe katika maeneo mbalimbali muhimu ya kijamii (Sanga, 2018). Makala haya yamechambua hadithi fupi simulizi kama sehemu ya fasihi simulizi ya Kiswahili ili kuonesha thamani za ujumi wa Kiafrika kwa ustawi wa jamii za Kiafrika. Utafiti uliozalisha makala haya ulikuwa wa kimaktaba na uwandani. Aidha, data zilikusanywa kwa kutumia mbinu za uchanganuzi matini na mahojiano. Utafiti ulitumia mkabala wa kitaamuli katika uchambuzi na uwasilishaji wa data. Aidha, data hizo pia zilichanganuliwa kwa kutumia misingi ya Nadharia ya Ujumi Mweusi.


Journal Identifiers


eISSN: 2546-2202
print ISSN: 0856-0129