Main Article Content

Dhima za Kisarufi na Kisemantiki za Viambajengo Vinavyohusika katika Uchanganuzi wa Tungo za Utendeka na Utendwa


Fredrick Emanuel Kuyenga

Abstract

Makala haya yamechunguza tungo za utendeka na utendwa katika lugha ya Kiswahili. Lengo ni kuweka wazi dhima za kisarufi na kisemantiki za viambajengo vinavyohusika katika tungo hizo. Hii ni kwa sababu, yapo madai miongoni mwa wanaisimu mbalimbali kwamba tungo hizi zinafanana katika miundo na uamilifu wake katika lugha kisarufi; yaani kiima katika tungo hizi kinahusishwa na kiathirika au na kithimu pekee (taz. Khamisi, 1972; Rugemalira, 1993 na Mkude, 2005). Iko haja ya kubainisha zaidi dhima za kisarufi na za kisemantiki za viambajengo vyote vinavyohusika katika tungo hizi ili kuweza wazi suala hili katika lugha ya Kiswahili. Data za utafiti huu zilikusanywa kutoka katika magazeti mawili (2) pamoja na watoataarifa kumi (10). Data zilipatikana kwa njia ya usomaji wa nyaraka pamoja na usaili. Uchanganuzi wa data umetumia misingi ya Mkabala wa Sarufi Leksia Amilifu ulioasisiwa na Bresnan na Kaplan mwishoni mwa miaka ya 1970. Matokeo yanaonesha kwamba tungo za utendeka na utendwa zinafanana na kutofautiana katika miundo na uamilifu wa viambajengo katika lugha ya Kiswahili. Kutokana na matokeo haya, inapendekezwa kwamba utafiti zaidi kama huu ufanyike katika lugha nyingine za Kibantu ambazo hazijafanyiwa utafiti ili kulinganisha na kutofautisha uamilifu wa viambajengo katika lugha ya Kiswahili na lugha nyingine. Makala haya yameweka wazi dhima za kisarufi na za kisemantiki za viambajengo vyote vinavyohusika katika tungo za utendeka na zile za utendwa katika lugha ya Kiswahili.


Journal Identifiers


eISSN: 2546-2202
print ISSN: 0856-0129