Main Article Content

Ulinganishi wa Ngeli za Nomino za Kipemba na Kingazija


Sauda Uba Juma

Abstract

Makala haya yanachunguza ulinganishi wa ngeli za nomino za Kipemba na Kingazija ili kubaini namna zinavyofanana na kutofautiana. Makala haya ni sehemu ya utafiti mpana uliofanywa wa kulinganisha kiisimu Kipemba na Kingazija kwa lengo la kubaini uhusiano wa kimnasaba uliopo miongoni mwake. Ulinganishi wa ngeli za nomino umejikita kwenye viambishi katika maumbo ya umoja na wingi. Data iliyotumika katika utafiti uliozaa makala haya ilikusanywa uwandani kupitia mbinu za hojaji na mahojiano. Ulinganishi wa ngeli za nomino unaweza kufanywa kwa kutumia mikabala mbalimbali kulingana na wanazuoni tofauti waliojaribu kuainisha ngeli za nomino. Hata hivyo, katika makala haya ulinganishi huo umefanywa kwa kuegemea kigezo cha kimofolojia. Lengo ni kubaini namna maumbo ya viambishi vya umoja na wingi vya Kipemba na Kingazija yanavyofanana na kutofautiana. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba Kipemba na Kingazija zinashabihiana katika mfumo wake wa ngeli za nomino. Hali hii inaashiria kwamba lahaja hizi zimetokana na lugha-mame moja.


Journal Identifiers


eISSN: 2546-2202
print ISSN: 0856-0129