Main Article Content
Viambishi-Ngeli katika Nomino za Pekee: Mifano kutoka katika Majina ya Mahali katika Kihaya
Abstract
Makala haya yanawakilisha uchambuzi wa kimofolojia, wa awali, wa majina ya mahali katika Kihaya, mojawapo ya lugha za Kibantu inayozungumzwa Kaskazini-Mashariki mwa Ziwa Nyanza, Tanzania. Kazi hii inalenga kubainisha viambishi-ngeli katika majina ya mahali, kudadisi utokezi wa viambishi-ngeli zaidi ya kimoja katika nomino moja, na kufafanua dhima zinazodokezwa katika viambishi-ngeli hivyo. Madai yanayoongoza makala haya ni kwamba viambishi-ngeli katika majina ya mahaliĀ hutokana na nomino za kawaida ambazo kwazo majina ya mahali huundwa.