Main Article Content

Mabadiliko Ya Kifonolojia Na Kimofolojia Wakati Wa Utohozi Wa Maneno Ya Kiarabu Katika Kiswahili: Mifano Kutoka Kamusi Ya Kiswahili Sanifu (Tuki 2004)


MMS Shembilu

Abstract

Mwingiliano wa lugha ya Kiswahili na Kiarabu una historia ndefu kidogo.  Inasemekana Waarabu walianza muwasala na 'Waswahili' tangu karne ya kwanza (BK) (Polome 1967:9). Kutokana na muwasala huo wa muda mrefu, lugha hizi mbili (Kiarabu na Kiswahili) zimeathiriana sana. Lakini kuna maoni kwamba Kiarabu kinaongoza katika kukiathari Kiswahili kimsamiati (Lodhi 2000). Hii ina maana kuwa Kiswahili kimekopa msamiati mwingi kutoka katika Kiarabu.

Katika ukopaji wa msamiati wa Kiarabu katika Kiswahili, baadhi ya maneno hayo yametoholewa ili yaendane na fonolojia na au mofolojia ya lugha ya Kiswahili. Wakati maneno hayo yakitoholewa kuna mabadiliko ya kifonolojia na kimofolojia ambayo huambatana na utohozi huo. Katika makala haya tunajaribu kuonyesha baadhi ya mabadiliko yaliyotokana na hali hiyo.

 


Journal Identifiers


eISSN: 0023-1886