Main Article Content
Dhima Ya Uradidi Katika Mawasiliano Ya Kiswahili: Uimarishaji Na Udhoofishaji Wa Maana
Abstract
Katika maisha ya kila siku binadamu wanahitaji kuwasiliana ili kutimiza mahitaji ya msingi na yale za ziada. Kutokana na upungufu wa msamiati unaohitajika kutaja kila dhana, watumiaji wa lugha hutumia mbinu mbalimbali za kuboresha msamiati uliopo ili ubebe dhana za ziada. Baadhi ya mbinu zitumiwazo ni uradidi. Uradidi ni dhana inayojitokeza katika lugha nyingi ikiwa na dhima tofauti. Katika lugha ya Kiswahili, tukiacha dhima nyingi nyingine kama zile zilizobainishwa na Ashton (1944:316-318), uradidi unaweza kutumika katika kuimarisha au kudhoofisha maana au kuongeza na kupunguza msisitizo wa dhana inayozungumziwa. Kwa hiyo, wakati mwingine mtumiaji wa lugha ya Kiswahili hulazimika kutumia mbinu ya uradidi ili kuwasilisha dhana ambayo ama haina msamiati unaojitegemea au mzungumzaji hajui msamiati unaofaa kutumika katika muktadha unaohusika. Dhana hii ya uradidi hujitokeza zaidi katika lugha ya mazungumzo ambapo wazungumzaji wanakuwa huru kutumia mbinu zozote wanazozijua ili kuwezesha mawasiliano yafanikiwe kwa kiwango kinachostahili. Katika makala haya tutaichunguza kwa makini dhana hii.