Main Article Content

Uzoefu wa Ufundishaji na Ujifunzaji wa Lugha ya Kiswahili nchini Uganda


Racheal Munyakiire

Abstract

Suala la ufundishaji na ujifunzaji wa lugha ya Kiswahili nchini Uganda limewashughulisha watalaamu mbalimbali (Kahaika, 2018; Kahaika, 2020; Jjingo, 2020). Wataalamu hao wanadai kuwa Kiswahili ni lugha ya kigeni nchini Uganda hasa kwa kuzingatia matumizi yake finyu  katika jamii. Licha ya watalaamu hao kukiri hivyo, bado haijaeleweka namna lugha ya Kiswahili inavyofundishwa nchini Uganda hususani  kwa kuzingatia mbinu zitumikazo. Hivyo, makala hii inabainisha namna lugha ya Kiswahili inavyofundishwa nchini huko kwa kuelezea  mbinu mbalimbali zinazotumiwa katika ufundishaji na ujifunzaji wake katika ngazi tofautitofauti na changamoto zinazolikumba zoezi  zima la ufundishaji na ujifunzaji wa lugha hiyo. Vivyo hivyo, makala hii inafafanua namna lugha ya Kiswahili ilivyofanikiwa nchini Uganda  kwa kubainisha nyanja mbalimbali ambako lugha hiyo inatumika. Pia, ili lugha ya Kiswahili ienee zaidi nchini Uganda, makala hii imetoa mapendekezo ambayo yakizingatiwa yatasaidia katika shughuli mbalimbali za ueneaji wa Lugha hiyo. Aidha, makala hii iliongozwa na Nadharia ya Upangaji wa Lugha ya Haugen (1983) inayosisitiza uteuzi wa lugha kisheria na pia utekelezaji wake kupitia shughuli  mbalimbali. Data za makala hii zilipatikana kwa kufanya udurusu wa nyaraka mbalimbali zinazopatikana maktabani na mtandaoni  pamoja na uzoefu wa mwandishi alionao katika ufundishaji wa lugha ya Kiswahili nchini Uganda.  


Journal Identifiers


eISSN: 0023-1886