Main Article Content

Ufinyaji wa Fursa za Kiswahili Nchini Tanzania: Uchunguzi Kifani wa Sera ya Lugha na Mpangolugha


Elishafati J. Ndumiwe
Elishafati J. Ndumiwe

Abstract

Mpangolugha nchini Tanzania huipa lugha ya Kiingereza hadhi ya juu, Kiswahili hadhi ya kati na lugha za kijamii hadhi ya chini (Msanjila,  2009; Rugemalira, 2013; Ndumiwe, 2019; Kawonga, 2023). Lugha iliyopewa hadhi ya juu hutumika katika shughuli rasmi kama vile  mahakama za juu, diplomasia, mikataba na shughuli za kimataifa. Fursa katika lugha hutegemea mawanda mapana ya matumizi ya  lugha inayobidhaishwa. Hata hivyo, lugha ya Kiswahili nchini Tanzania imepewa mawanda finyu katika shughuli rasmi ikilinganishwa na  lugha ya Kiingereza. Kwa hiyo, utafiti huu unachunguza namna mpangolugha na sera ya lugha vinavyofinya fursa za Kiswahili nchini Tanzania. Data za makala hii zimekusanywa maktabani na uwandani. Kwa upande wa maktabani, data zilikusanywa kutoka andiko la Sera  ya Utamaduni (WEU, 1997) kwa kutumia mbinu ya usomaji wa matini. Aidha, kwa upande wa uwandani, data zilikusanywa kutoka  kwa wahitimu wa ualimu katika Kiswahili, wafasiri, wakalimani na walimu wa shule za sekondari kwa kutumia mbinu ya usaili. Nadharia  ya Ikolojia ya Kiisimu iliyoasisiwa na Wendel (2005) ilitumika katika kuchanganua data za utafiti huu. Utafiti huu umebaini kuwa mpangolugha na sera ya lugha huminya fursa katika Kiswahili kama vile tafsiri, ukalimani, ufundishaji wa Kiswahili kwa wageni, uhariri na  uchapishaji katika Kiswahili. Utafiti huu unapendekeza kuandaliwa kwa sera ya lugha na mpangolugha mpya ili kuiweka lugha ya  Kiswahili katika darajia la juu. Suala hilo litaongeza fursa za kiuchumi katika lugha ya Kiswahili. 


Journal Identifiers


eISSN: 0023-1886