Main Article Content

Ala za Kisintaksia katika Ufafanuzi wa Dhima za Viambajengo vya katika Lugha ya Kiswahili


Fabiola Hassan
Luinasia Kombe

Abstract

Makala hii inahusu ala za sintaksia na namna ambavyo zinaweza kutumika katika ufafanuzi wa dhima za kisarufi za viambajengo vya sentensi za lugha ya Kiswahili. Licha ya ufafanuzi wa kina uliofanywa kuhusu mada hii, bado kuna masuala ambayo hayako bayana au yana utata. Mathalani, kuna utata juu ya dhima za kisarufi za viambajengo vinavyotokea mara baada ya kitenzi. Haiko wazi iwapo kila kiambajengo kinachotokea katika nafasi hiyo ni yambwa au la. Kwa hiyo, makala hii inalenga kufafanua ala mbalimbali za kisintaksia na kueleza namna ala hizo zinavyoweza kutumika kufafanua dhima za kisarufi za viambajengo vya sentensi za lugha ya Kiswahili ili kutatua utata unaoweza kujitokeza kuhusu dhima hizo. Data za makala hii zimepatikana kwa mbinu ya hojaji pamoja na usaili na kuchambuliwa kwa kutumia misingi ya Sarufi Leksia Amilifu. Kwa ujumla, tumebaini kuwa kuna ala kuu tano za kisintaksia katika lugha ya Kiswahili. Ala hizo ni pamoja na ukategoria wa neno, viambajengo vya maneno, viambishi, vijineno maalumu na kiimbo. Ala hizi ndizo zinazowasaidia wanasintaksia kufafanua dhima mbalimbali za kisarufi kama vile kiima, yambwa, yambiwa, yambwaϴ, oblikyumahali na chagizo. Ala za kisintaksia ni nyenzo muhimu katika ufafanuzi wa dhima za kisarufi za viambajengo vya sentensi za Kiswahili.


Journal Identifiers


eISSN: 0023-1886
 
empty cookie