Main Article Content

Mofimu za Udogoshi na Ukuzishi katika Mfumo wa Ngeli za Nomino za Lugha ya Kibena: Mkabala wa Kimofolojia


Faraja Mwendamseke
Saul S. Bichwa

Abstract

Makala hii inachunguza mofimu za udogoshi na ukuzishi katika mfumo wa ngeli za nomino za Kibena. Katika mfumo wa ngeli za nomino dhana za udogoshi na ukuzishi hudhihirika katika lugha nyingi za Kibantu. Aidha, mfumo wa ngeli katika Mame-Bantu unatofautiana na ule wa lugha nyingi za Kibantu. Kwa hiyo, ngeli inayobeba mofimu hizo si suala la kimajumui katika lugha za Kibantu. Lengo la makala hii ni kuonesha jinsi mofimu za udogoshi na ukuzishi zinavyojidhihirisha katika Kibena. Data za makala hii zilikusanywa kwa mbinu ya upitiaji nyaraka. Aidha, data hizo zilichambuliwa kwa mkabala wa maelezo. Mkabala wa Viambishi Awali vya Nomino wa uainishaji wa ngeli kimofolojia ndio uliotumika kubainisha maumbo yanayoonesha udogoshi na ukuzishi. Makala hii inadhihirisha kuwa kuna upekee katika mfumo wa ngeli za udogoshi na ukuzishi katika lugha ya Kibena ambao ni tofauti kidogo na baadhi ya lugha nyingine za Kibantu. Matokeo yanaonesha kuwa katika lugha ya Kibena viambishi vya udogoshi vinapatikana katika ngeli ya 12/13 (-ha-/-tu-) na ukuzishi ni ngeli ya 5/6 (-li-/-ma-) pamoja na ngeli ya 20/6 (-gu-/-ma-). Aidha, viambishi hivi huweza kuambatana na dhima nyingine. Hata hivyo, katika utokeaji wa viambishi hivi katika ngeli, inaonesha kuwa katika miktadha mingine kuna mchakato wa uongezaji wa kiambishi ngeli kingine au ubadilishanaji wa kiambishi ngeli.


Journal Identifiers


eISSN: 0023-1886
 
empty cookie