Main Article Content

Ala za Kisintaksia katika Ufafanuzi wa Dhima za Viambajengo vya katika Lugha ya Kiswahili


Fabiola Hassan
Luinasia Kombe

Abstract

Makala hii inahusu ala za sintaksia na namna ambavyo zinaweza
kutumika katika ufafanuzi wa dhima za kisarufi za viambajengo vya
sentensi za lugha ya Kiswahili. Licha ya ufafanuzi wa kina uliofanywa
kuhusu mada hii, bado kuna masuala ambayo hayako bayana au yana
utata. Mathalani, kuna utata juu ya dhima za kisarufi za viambajengo
vinavyotokea mara baada ya kitenzi. Haiko wazi iwapo kila kiambajengo
kinachotokea katika nafasi hiyo ni yambwa au la. Kwa hiyo, makala hii
inalenga kufafanua ala mbalimbali za kisintaksia na kueleza namna ala
hizo zinavyoweza kutumika kufafanua dhima za kisarufi za viambajengo
vya sentensi za lugha ya Kiswahili ili kutatua utata unaoweza kujitokeza
kuhusu dhima hizo. Data za makala hii zimepatikana kwa mbinu ya hojaji
pamoja na usaili na kuchambuliwa kwa kutumia misingi ya Sarufi Leksia
Amilifu. Kwa ujumla, tumebaini kuwa kuna ala kuu tano za kisintaksia
katika lugha ya Kiswahili. Ala hizo ni pamoja na ukategoria wa neno,
viambajengo vya maneno, viambishi, vijineno maalumu na kiimbo. Ala
hizi ndizo zinazowasaidia wanasintaksia kufafanua dhima mbalimbali za
kisarufi kama vile kiima, yambwa, yambiwa, yambwaϴ, oblikyumahali na
chagizo. Ala za kisintaksia ni nyenzo muhimu katika ufafanuzi wa dhima
za kisarufi za viambajengo vya sentensi za Kiswahili.


Journal Identifiers


eISSN: 0023-1886