Main Article Content

Kiswahili na Wadau: Fursa na Changamoto kwa Maendeleo Endelevu


John G. Kiango

Abstract

Lengo la makala hii ni kujadili fursa na changamoto kwa maendeleo
endelevu ya lugha ya Kiswahili, hususan baada ya Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni - UNESCO
kutangaza Siku ya Maalumu ya Kiswahili duniani. Kutangazwa kwa siku
hii kunatoa fursa kwa wadau wa Kiswahili katika ngazi zote za kitaifa na
kimataifa kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana na maendeleo ya
Kiswahili. Katika makala hii, pamoja na masuala yaliyolengwa,
mwandishi anatoa shukurani zake kwa asasi mbalimbali za kimataifa
ambazo zimeshiriki kwa namna tofauti katika mchakato wa kufanikisha
hatua ya kutangazwa tarehe 7 Julai kuwa siku maalumu ya Kiswahili
duniani. Makala hii inajadili kwa ujumla, majukumu na mchango wa
wadau mbalimbali katika maendeleo ya Kiswahili kwa kudokeza fursa na
changamoto katika maendeleo hayo. Mtafiti anahitimisha kwa kusisitiza
kuwa jukumu la kuendeleza lugha ni la taasisi zote za elimu, hususan
vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi. Kutokana na changamoto kubwa ya
kifedha, uzalendo uwekwe mbele ili kufanikisha malengo ya kukuza
Kiswahili.


Journal Identifiers


eISSN: 0023-1886