Main Article Content

Dhima ya Ngoma katika Tamthiliya ya Kiswahili ya Kimajaribio: Mfano kutoka Lina Ubani (1984)


Aneth Kasebele

Abstract

Makala hii inachunguza dhima ya ngoma katika tamthiliya ya Kiswahili ya kimajaribio. Tafiti kuhusu matumizi ya ngoma katika tamthiliya  ya Kiswahili ya kimajaribio zimeishia katika ngazi ya kubainisha tu pasi na kuchambua dhima zake. Kitendo cha kubainisha tu bila  kuchambua dhima za ngoma katika tamthiliya ya Kiswahili ya kimajaribio hakioneshi umuhimu wa kipengele hicho cha kifasihi simulizi  katika kazi za fasihi andishi. Data za makala hii zilipatikana maktabani kwa kusoma tamthiliya ya Lina Ubani kisha kuchambua dhima ya  ngoma. Uchambuzi wa data za makala hii umeongozwa na Nadharia ya Uamilifu. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa ngoma ina  dhima za kifani na kimaudhui katika tamthiliya ya Kiswahili ya kimajaribio.


Journal Identifiers


eISSN: 0023-1886