Main Article Content
Ulinganishi wa Motifu Zinazoibuliwa na Majagina Wawili Maarufu: Mfano kutoka Biblia Takatifu na Utendi wa Fumo Liyongo
Abstract
Suala la motifu katika kazi ya fasihi ni la msingi kwani hubainisha kiwango cha mwingiliano wa vipengele mbalimbali vya kifasihi ili kuleta msisitizo, kukuza maudhui pamoja na kuendeleza dhamira mbalimbali. Makala hii imelinganisha motifu za mashujaa Fumo Liyongo na Samsoni. Uchunguzi wa mashujaa ulifanyika katika maktaba za umma na vyuo vikuu nchini Kenya. Sampuli iliyohusishwa ilikuwa ni majagina wawili ambao ni Samsoni kutoka katika Biblia Takatifu na Fumo Liyongo kutoka katika Utendi wa Fumo Liyongo. Kwa upande mwingine, uchanganuzi wa data ulihusisha mbinu ya kimaelezo. Isitoshe, uchanganuzi wa makala hii uliongozwa na Nadharia ya Ruwaza ya Shujaa iliyoasisiwa na Campbell (2004). Msukumo wa ulinganishi wa motifu za majagina hawa unatokana na madai kuwa majagina hutofautiana kutokana na tofauti za kitamaduni. Kwa majagina teule, hali hii ni tofauti kwa sababu, licha ya kuwa waliishi katika mazingira na vipindi tofauti, wanaonekana kuibua motifu zinazoshabihiana. Makala hii imewatathmini mashujaa hawa na kubaini kuwa wamefungamana na motifu za ujumbe, kuogofya na kustaajabisha, safari, kifo, hila na usaliti. Hivyo, matokeo ya uchunguzi wa motifu za mashujaa yamebainisha kuwa kwa kiwango kikubwa, motifu zao zinafanana na kuingiliana. Katika Utendi wa Fumo Liyongo, Fumo Liyongo alikuwa maarufu sana kutokana na vitendo vyake vya ajabu katika jamii alimoishi. Vilevile, Samsoni amedhihirika kama mtu wa ajabu na mwenye uwezo na mamlaka yanayomfanya aogopwe kutokana na matendo yake mengi ya kiuhalisiaajabu anayoyatenda.