Main Article Content

Ujitokezaji wa Kelele katika Kipimo cha Mizani na Dunia Uwanja wa Fujo


Winifrid Mligo
Aldin Mutembei

Abstract

Makala haya yanachambua ujitokezaji wa kelele kama mbinu katika uchambuzi wa kazi za kifasihi za Kiswahili. Kelele ni aina ya sauti, na ingawa sauti kwa ujumla wake imeangaliwa na wachambuzi wa fasihi kama mojawapo ya vijenzi vya kazi za fasihi, lakini kelele kama aina ya sauti haikupewa uzito unaoeleza dhima yake katika kuiumba kazi ya fasihi. Mara nyingi kelele imeachwa kama kipengele kisicho na mchango wa maana katika kuwapo kwa kazi ya kifasihi. Katika Makala haya tumeongozwa na Nadharia ya Korasi katika kubainisha na kuchambua dhima ya kelele kutoka katika riwaya mbili za Kiswahili ambazo ni Kipimo cha Mizani (2004) na Dunia Uwanja wa Fujo (2007). Data zinazohusu kelele zilikusanywa kutoka katika kazi hizi na kuzingatia nafasi yake katika kujenga maana na dhamira mbalimbali za kazi husika. Uchambuzi wa Kikorasi unatuonesha kuwa kelele ni kipengele muhimu kiuchambuzi ambacho kinasaidia katika uelewekaji wa kazi za fasihi. Makala yanahitimisha kwa kutoa rai kuwa ujitokezaji wa kelele katika kazi za fasihi uangaliwe kwa uzito wake kwani unabeba dhima muhimu katika uelewekaji wa kazi za fasihi.


Journal Identifiers


eISSN: 0023-1886