Main Article Content

Misemo ya ‘Vyuma Vimekaza’1: Uchambuzi wa Mtindo na Dhima yake


Shani Omari Mchepange

Abstract

Misemo ni kipera kimojawapo cha semi. Ni fungu la maneno lenye maana maalumu, ujumbe kwa muhtasari na ukweli fulani. Misemo mingi huibuka na kutumika kulingana na muktadha fulani wa kijamii. Hivi karibuni (kuanzia mwaka 2016) kumezuka misemo anuwai miongoni mwa Watanzania yenye kuhusisha neno ‘vyuma’ ili kuwasilisha hali au ujumbe fulani. Miongoni mwa misemo hiyo ni ‘Vyuma Vimekaza’, ‘Vyuma Vimebana’, ‘Vyuma Vimeachia’ na kadhalika. Lengo la makala hii ni kujadili maana ya misemo hiyo miongoni mwa watumiaji wake katika muktadha wa sasa nchini Tanzania. Aidha, makala inachambua mitindo iliyotumika katika misemo hiyo na dhima zake. Misemo hii imekusanywa kutoka kwa jamii (baadhi ya watumiaji wa misemo hii), mitandaoni na magazetini. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kwamba misemo hii inatumia mitindo mbalimbali na ina dhima kadhaa kifasihi na kijamii.


Journal Identifiers


eISSN: 0023-1886
 
empty cookie