Main Article Content

Mofolojia katika Uingizaji wa Vinyambuo Vitenzi kwenye Kamusi: Mifano kutoka Kamusi ya Kiswahili Sanifu Toleo la Tatu (2013)


Fatuma Abdallah

Abstract

Suala la kanuni za uingizaji wa vinyambuo vitenzi limejadiliwa na wataalamu kama vile Mdee (1990, 1995), Kiango (1996, 2006, 2015), Howard (2003), Prinsloo (2009) ambao wameeleza kanuni za kileksikografia zinazopaswa kuzingatiwa wakati wa kuingiza vinyambuo vitenzi katika kamusi. Kanuni hizo ni kuingiza vinyambuo vitenzi kama kidahizo kikuu au kuviingiza kama kidahizo mfuto. Hata hivyo, wataalamu hawa hawaelezi chochote kuhusu kanuni za kimofolojia zinazozingatiwa katika uingizaji wa vinyambuo vitenzi katika kamusi kama vile kanuni za unyambulishaji ingawa wanakubaliana kwamba vinyambuo vitenzi hutokana na mchakato wa unyambulishaji. Makala hii inachambua na kufafanua kanuni za kimofolojia za kuzingatia wakati wa kuingiza vinyambuo vitenzi katika kamusi za Kiswahili. Data zilizotumika katika makala hii zinatoka katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu, (TUKI 2013) na uchanganuzi wa data umezingatia nadharia ya kileksika.


Journal Identifiers


eISSN: 0023-1886