Main Article Content
Mambo Yanayochangia Makutano ya Wazungumzaji wa Lahaja za Kiswahili katika Upwa wa Afrika Mashariki
Abstract
Makala hii inachunguza mambo yanayosababisha makutano ya wazungumzaji wa lahaja za Kiswahili katika upwa wa Afrika Mashariki na visiwa vyake. Data ya makala hii imekusanywa uwandani kwa kutumia mbinu za usaili na mahojiano ya majopo. Uchambuzi na uchanganuzi wa data umeongozwa na Nadharia ya Mwachano na Makutano ya Wabantu Kiisimu ya Massamba (2007). Kwa mujibu wa nadharia hii, mijongeo ya watu iliyotokea waliposambaa kutoka eneo kiini kuja Mashariki ilisababisha lugha zao kuachana na kwa kutokana na muwasala wa muda mrefu uliochangiwa na mitagusano mbalimbali ya kijamii ulisababisha lugha zao zikaanza kukutana tena. Katika uchunguzi huu tumegundua kwamba kuna mambo kadhaa ambayo yanachangia makutano ya wazungumzaji wa lahaja za Kiswahili katika upwa huu. Mambo hayo ni pamoja na shughuli za biashara, uvuvi, kuoleana, kupigana vita, safari za bahari, na kadhalika. Kwa ujumla, makutano haya yanatokana na hali ya kuwapo kwa muwasala wa muda mrefu baina ya wazungumzaji wa lahaja za Kiswahili katika upwa huu.