Main Article Content

Ulinganishi wa Mfumo wa Sauti Katika “Lugha” za Mara Kaskazini


Boniphace M. Alphonce

Abstract

Makala hii inahusu ulinganishi wa mfumo wa sauti katika “lugha” za Mara Kaskazini. Sauti zilizolinganishwa ni konsonanti na irabu. Ulinganishi huu umezingatia Nadharia ya Isimuhistoria na Isimulinganishi katika kuonesha uhusiano wa “lugha” zilizochunguzwa. Lengo la ulinganishi wa “lugha” hizi ni kubaini kama kuna mfanano au tofauti miongoni mwake. Matokeo  yaliyotokana na data kutoka uwandani yamedhihirisha mfanano mkubwa wa “lugha” hizi za Mara Kaskazini katika mfumo wa sauti. Matokeo haya  yanatushawishi tuzichukulie “lugha” hizi kama ni lahaja zinahusiana kwa karibu, na pengine zimetokana na lugha-chanzi moja na sio lugha  zinazojitegemea kama zinavyotazamwa kiisimujamii.

Journal Identifiers


eISSN: 0023-1886