Main Article Content
Dhana ya Utendaji na Usambaaji wa Nyimbo kwa Wakati: Mifano kutoka Nyimbo za Kiswahili
Abstract
Nyimbo ni mpangilio maalumu wa maneno fasaha, yanayoimbwa na mtu mmoja au kikundi katika shughuli mbalimbali. Nyimbo hizo hubeba dhima ya kuelimisha jamii kwa kuwa hutumika kutoa mafunzo mbalimbali kwa jamii. Tunapoziangalia nyimbo za Kiswahili, hatuwezi kwa haraka kugundua namna zinavyoweza kusambaa kiutendaji kwa wakati hadi hapo utakapoziangalia kupitia katika dhana ya wakati kwa kuyatilia mkazo maneno ya nyimbo hizo. Tumegundua kuwa, maneno ya nyimbo yanayowasilishwa na kusambazwa kwa kughanwa, kutambwa na hata kwa kutongolewa au kusemwa huwa yanakwenda sambamba na dhana nzima ya utendaji wa wakati. Hivyo basi, makala yetu itaichanganua mifano kutoka nyimbo za jamii kwa lengo la kuonesha jinsi zinavyotumiwa katika utendaji na zinavyosambazwa kwa nyakati tofauti bila kuathiri maudhui ya nyimbo zenyewe. Makala itazichambua baadhi ya nyimbo za Kiswahili za jamii kama mifano ili kuonesha jinsi zinavyoingiliana na kusambazwa kwa wakati kutoka jamii moja hadi nyingine, kupitia kwa fanani tofauti na kisha kurejeshwa kwa jamii kupitia fanani walewale au kupitia vifaa vya kielektroniki. Kwa upande mwingine, makala itatumia nyimbo za Kiswahili ili kuthibitisha mwingiliano na msambao wa nyimbo hizo kiutendaji kwa wakati.