Main Article Content
Utata kuhusu Dhana na Chimbuko la Wahadimu katika Kisiwa cha Unguja
Abstract
Lengo la makala haya ni kujadili utata wa dhana ya Wahadimu na chimbuko lao linaloibuka kutokana na mitazamo ya wataalamu mbalimbali. Data za makala haya zimepatikana kupitia usaili na majadiliano ya majopo ya wazungumzaji wa Kimakunduchi na Unguja na kujadili kwa muhtasari chimbuko la Wahadimu. Kwa muda mrefu dhana ya Wahadimu imekuwa ikijadiliwa kwa mitazamo tofautitofauti kama inavyobainishwa na wataalamu mbalimbali wakiwemo wanahistoria, wanaisimu na wanaethnoisimu. Ili kuweza kuielewa vyema dhana hiyo, ni vyema kwanza tukaelezea kwa muhtasari kuhusu maeneo ya Tumbatu na Makunduchi pamoja na wakazi wake.