Main Article Content

Uhistoria katika Riwaya ya Kiswahili: Mifano kutoka riwaya za ‘Ndoto ya Ndaria’, ‘Gamba la Nyoka’ na ‘Miradi Bubu ya Wazalendo


Wallace Mlaga

Abstract

Makala haya yanaangalia kwa kina namna uhistoria unavyojitokeza katika riwaya ya Kiswahili. Makala haya yalichochewa na makala mengine yaliyokuwa yanaangalia namna ambavyo riwaya ya Kiswahili ilivyo na uwezekano wa kutumika katika kufundishia historia1. Kutokana na makala hayo, iliibuka shauku ya kuonesha kwa mifano dhahiri namna ambavyo uhistoria unajitokeza katika riwaya ya Kiswahili. Makala haya yamejiegemeza katika hoja kuwa uhistoria katika riwaya ya Kiswahili unajitokeza kwa kuegemea katika misingi mikuu ya mambo matatu; falsafa ya historia, Nadharia ya Uhalisia, na Nadharia ya Uhistoria Mpya. Misingi hii mitatu ndiyo inayoifanya riwaya ya Kiswahili na riwaya kwa ujumla ifae kutumika kufundishia historia. Hivyo basi, makala haya yamejikita katika kuonesha namna ambavyo misingi hii mitatu inadhihirisha uhistoria katika riwaya ya Kiswahili. Makala yanamalizia kwa kuacha swali la mjadala kama kuna tatizo lolote la kufanya uhakiki wa fasihi kwa kuegemea katika misingi tu ya uhistoria iliyobainishwa katika makala haya.

Journal Identifiers


eISSN: 0023-1886