Main Article Content
Usukuku katika ujifunzaji wa lugha ya Kiswahili katika jamii ya wakinga
Abstract
Usukuku ni dhana inayotumika sana katika taaluma ya isimu matumizi, hasa katika kipengele cha ujipatiaji na ujifunzaji wa lugha ya pili na au ya kigeni, ikiwa na maana ya ukomo wa mtu kuendelea kujipatia lugha baada ya balehe (Long, 1997). Makala haya kwa hiyo yanafasili na kuainisha dhana hii katika muktadha wa Kiswahili. Pili, yanapendekeza baadhi ya mbinu ambazo zinaweza kutumiwa na walimu wanaofundisha lugha ya pili ili kuwasaidia wajifunzaji kuondokana na tatizo la usukuku. Swali linaloibuliwa na kujibiwa na makala haya ni je, kuna ukomo wa ujipatiaji lugha kama wanavyodai Long (1997), Lardiere (1998) na Jiang (2000)?