Main Article Content

Athari za uhamishaji wa sarufi ya Kiluo kwenye upatanisho wa sarufi ya Kiswahili


Carolyne Oduor
K. Simala Inyani
M. John Kobia

Abstract

Makala haya yanaonesha athari za uhamishaji wa sintaksia ya Kiluo kwa upatanishi wa sarufi ya Kiswahili. Utafiti ulifanywa baada ya mtafiti kubainisha kuwa maandishi ya wanafunzi ambao lugha yao ya kwanza ni Kiluo yalikuwa na makosa mengi ya kisarufi, hali ambayo ilikuwa inaathiri ujifunzaji wa Kiswahili kama lugha ya pili. Uhamishaji wa sarufi ya Kiluo huathiri upatanishi wa kisarufi katika Kiswahili kwa sababu kanuni za lugha hizi mbili ni tofauti. Maneno mengi ya Kiswahili huambishwa. Viambishi vya upatanishi hutokana na ngeli ya nomino kuu katika sentensi na viambishi hivi ndivyo huonesha uhusiano wa maneno katika sentensi. Kwa upande mwingine, lugha ya Kiluo ina maneno machache ambayo huambikwa. Viambishi vya upatanishi hutumiwa tu kikundi nomino kinapoundwa na kiwakilishi. Athari ya uhamishaji wa sarufi ya Kiluo kwenye sarufi ya Kiswahili ilibainika katika viwango vitatu vya kisarufi: ngeli, nafsi na idadi. Utafiti uliongozwa na nadharia ya Umilikifu na Uhusisho (Chomsky, 1981). Nadharia hii huonesha hali ya vipashio fulani vya kisarufi kutawala vipashio vingine katika tungo.

Journal Identifiers


eISSN: 0023-1886