Kioo cha Lugha https://www.ajol.info/index.php/kcl
Kioo cha Lugha is an international journal published by the Institute of Kiswahili Studies (IKS). The journal is devoted to the publication of papers on Kiswahili language, linguistics and literature and other African languages. It promotes critical discussions and reviews, especially on contemporary issues regarding language and literature. The journal also publishes short pieces of fiction and poems. It is published annually but from 2021 it will be published bi-annually.

Journal website: https://journals.udsm.ac.tz/index.php/kcl

University of Dar es Salaam en-US Kioo cha Lugha 0856-552X Copyright is owned by the journal. Usukuku wa Ukolonia katika Mjadala wa Lugha ya Kufundishia nchini Tanzania https://www.ajol.info/index.php/kcl/article/view/286663
Makala hii inahusu usukuku wa ukolonia unaotawala fikra za wasomi katika mjadala wa lugha ya kufundishia nchini Tanzania. Lengo lake  ni kueleza kwa nini mapendekezo ya kubadilisha lugha ya kufundishia kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili yanapata ukinzani miongoni mwa wasomi nchini Tanzania. Data zilitokana na maoni ya wasomi kupitia kundi la WhatsApp la UDASA-MUCE. Kiunzi cha Ubadaukoloni  kinachohoji ukamilifu wa ukombozi uliopatikana katika nchi nyingi zilizowahi kutawaliwa kimetumika kuongoza utafiti huu. Matokeo  yanaonesha kwamba kuna usukuku wa ukolonia miongoni mwa wanazuoni unaoathiri fikra zao kuhusu lugha ya kufundishia licha ya  juhudi za kuwazindua. Kwa hiyo, ukombozi dhidi ya ukolonia wa maarifa hasa miongoni mwa wasomi ni muhimu na ni suala linalopaswa  kushughulikiwa kwa hatua za dharura ili kunusuru ubora wa elimu nchini Tanzania. Pendekezo ni kwamba serikali itumie madokezo ya  sera yanayotokana na tafiti za kisayansi kwa ajili ya kufanya maamuzi kuhusu lugha katika elimu.
Gervas A. Kawong Copyright (c) 2025 2025-01-16 2025-01-16 22 1 1 19 Ruwaza ya Kiidadi katika Ufafanuzi wa Vidahizo vya Kiantonimu katika Kamusi: Tathmini ya Kamusi Teule https://www.ajol.info/index.php/kcl/article/view/286664
Maana za vidahizo katika kamusi huelezwa kwa kutumia mbinu mbalimbali. Miongoni mwa mbinu hizo ni matumizi ya antonimu ambazo  hutumika zaidi kufafanua vidahizo vya kamusi za lugha moja kwa sababu walengwa wake huhitaji kupata maana kamilifu zote zinazotafutwa. Kwa msingi huo, antonimu zote zinazohusu kidahizo hutakiwa kuingizwa katika kidahizo husika kwa kufuata utaratibu. Ujitokezaji wa antonimu katika kamusi sio wa kiholela bali huzingatia uhusiano wa kimaana kati ya kidahizo na antonimu husika.  Uhusiano huo ndio huamua idadi na aina ya antonimu zinazopaswa kuambatana na kidahizo, hivyo, kuunda ruwaza fulani ambazo  huitwa ruwaza za kiidadi. Kuwapo kwa ruwaza hizo kumechangia kufanyika kwa utafiti huu unaotathmini kujitokeza kwa ruwaza za  kiidadi katika ufafanuzi wa kiantonimu wa vidahizo vya kamusi wahidiya za Kiswahili. Nadharia Jumuishi ya Leksikografia imetumiwa  katika uchambuzi wa data za makala hii. Data za zilikusanywa kutoka katika Kamusi Kuu ya Kiswahili toleo la tatu (yaani KKK3) kwa  kutumia mbinu ya uchambuzi wa matini. Jumla ya vidahizo 379 vimebainika kutumia antonimu katika ufafanuzi wake na kuunda ruwaza  tano za kiidadi zinazohusu umoja, uwili, utatu, unne na utano kutegemea idadi ya antonimu zilizotumika kuvifafanua vidahizo husika.
Jeremiah S. Andrew Mussa M. Hans Copyright (c) 2025 2025-01-16 2025-01-16 22 1 20 35 Athari za Kinyarwanda katika Ufundishaji na Ujifunzaji wa Kiswahili katika Shule Teule za Sekondari Wilayani Gakenke, Rwanda https://www.ajol.info/index.php/kcl/article/view/286665
Makala hii inachunguza jinsi Kinyawanda kinavyoathiri ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili. Watoataarifa 24 ambao ni wanafunzi 18,  walimu 3 pamoja na wakuu wa masomo 3, walitumiwa kuwa vyanzo vya taarifa. Data hizo zilikusanywa kupitia mahojiano, ushuhudiaji  pamoja na udurusu wa nyaraka. Nadharia ya Utabia iliyoasisiwa na Skinner mwaka 1950 ndiyo iliyoongoza utafiti huu. Matokeo  yanaonesha kwamba wanafunzi wanachanganya Kinyarwanda na Kiswahili kwa kuwa lugha hizi zina mfanano wa karibu kimatamshi,  kiotografia na kisemantiki. Hivyo basi, makala hii inapendekeza yafuatayo: mosi, kuwe na vitabu vya ziada na kiada shuleni. Pili,  ufundishaji wa Kiswahili uwe wa lazima kuanzia shule za chekechea hadi vyuoni. Tatu, Kiswahili kifundishwe katika michepuo yote kama  ilivyo kwa lugha ya Kiingereza. Mwisho, kuwe na mijadala na midahalo shuleni ili kuboresha kiwango cha lugha ya Kiswahili miongoni   mwa wanafunzi.
Martin H. Ikuramutse Vivens Niyotugira Pascal Sebazungu Copyright (c) 2025 2025-01-16 2025-01-16 22 1 36 48 The Interface between Intellectual Property Rights and Linguistics under the Laws of Tanzania https://www.ajol.info/index.php/kcl/article/view/286667
The intellectual property rights (IPR) system transcends many socioeconomic aspects ranging from human creative processes and the
manner they are expressed, and thereby, new words are formed for newly created products. Nevertheless, the operational intersections  of IPR and linguistics have not been fully explored and elaborated on in the national laws. Under the patent law, generating new technical  ideas and products necessitates creating new words or expressions. The contexts for using certain words to indicate the source  of products and services have a regulatory effect on trademark law. Equally important are the translation rights under copyright  law, which contribute to the development of new terminologies. This article explores the linkages of IPR and language development  using a qualitative assessment model to examine the interplay of IPR and language development in the context of the laws of Tanzania. It  addresses the inherent linguistic mischiefs and controversies arising from a misalignment of the etymological conception of words as  they are perceived under the lens of IPR and linguistics. Consequently, it establishes that there is a significant contribution of IPR in  language growth and that the operational and regulatory proximity of the two seemingly distant fields requires a reexamination.  Ultimately, this article underscores the necessity of including IPR modules in language studies and engaging language experts during the IPR registration process and dispute settlement.
Saudin J. Mwakaje Copyright (c) 2025 2025-01-16 2025-01-16 22 1 49 69 Uchambuzi wa Mashartizuizi katika Muundo wa Silabi za Kichasu https://www.ajol.info/index.php/kcl/article/view/286668
Makala hii imechunguza muundo wa silabi za lugha ya Kichasu kwa kuzingatia uchambuzi wa mashartizuizi ya Kichasu. Lengo la makala hii ni kubainisha miundo ya silabi za lugha hiyo. Utofauti wa udhihirikaji wa miundo ya silabi katika lugha mbalimbali za Kibantu ndio  umechagiza kufanyika kwa utafiti huu. Kutokana na tafiti mbalimbali, kila lugha huwa na mpangilio tofauti wa mashartizuizi na ujitokezaji  wa miundo yake huweka mipaka katika miundo ya silabi zake katika maneno. Data zilikusanywa kwa kutumia upitiaji  maandiko pamoja na masimulizi kutoka kwa watoataarifa. Data zilichanganuliwa kwa mkabala wa kitaamuli ambapo mbinu ya  uchanganuzi kimada imetumika. Uchanganuzi wa data uliongozwa na misingi ya Nadharia ya Umbo Upeo (1993). Matokeo yanaonesha  kwamba Kichasu kina jumla ya miundo kumi na mmoja ya silabi inayokubalika kisarufi. Miundo hiyo ni ya silabi nyepesi na ya silabi nzito.
Rabiel Fadhili Faraja Mwendamseke Copyright (c) 2025 2025-01-16 2025-01-16 22 1 70 89 Mitanziko ya Wahusika katika Riwaya Teule za Euphrase Kezilahabi https://www.ajol.info/index.php/kcl/article/view/286669
Watunzi wa kazi mbalimbali za fasihi huumba wahusika kwa ustadi mkubwa kwa lengo la kubeba maudhui na kuyafikisha kwa hadhira husika. Wahusika hao hubebeshwa fikra na tafakuri zinazoonesha hisia za mwandishi zinazoambatana na hali fulani katika kutoa  maamuzi ya tafakuri yake. Miongoni mwa mambo hayo ni mitanziko ambayo hubainika kupitia matendo wafanyayo wahusika hao.  Mitanziko hiyo husababisha wahusika kuchukua maamuzi ya kufanya au kutokufanya jambo fulani. Hivyo, makala hii inabainisha sababu  za mitanziko ya wahusika katika riwaya teule za Euphrase Kezilahabi ambazo ni Rosa Mistika (1971) na Kichwamaji (1974). Shabaha ya  kubainisha sababu hizo kwa mwegamo wa kifasihi ni kuthibitisha kwamba fasihi ni zao la jamii na kwamba mitanziko inayowakumba  wahusika katika riwaya hizo, ni usawiri wa wahusika halisi katika jamii, wanaokumbwa na mitanziko ya namna hiyo katika maisha yao ya  kila siku. Data za utafiti huu zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya usomaji matini. Misingi miwili ya Nadharia ya Udhanaishi ilitumika katika  uchunguzi, uchanganuzi na uwasilishaji wa matokeo ya makala hii. Matokeo yanaonesha kwamba mitanziko inayowakumba  wahusika katika riwaya teule inatokana na sababu kuu tatu, ambazo ni: za kijamii, kiutamaduni na kifalsafa.
Adria Fuluge Copyright (c) 2025 2025-01-16 2025-01-16 22 1 90 111 Matumizi ya Fantasia katika Fasihi ya Kiswahili Yanavyoibua, Kujenga na Kuwasilisha Dhamira https://www.ajol.info/index.php/kcl/article/view/286670
Makala hii imechunguza namna kipengele cha fantasia katika fasihi ya Kiswahili kinavyoibua, kujenga na kuwasilisha dhamira. Lengo la makala hii ni kuchunguza namna kipengele cha fantasia kinavyotumika kuibua, kujenga na kuwasilisha dhamira katika riwaya ya  Kiswahili. Data za msingi zilipatikana katika riwaya teule ya Kusadikika kwa mbinu ya usomaji makini. Nyaraka zilizotumika kufafanua na kuthibitisha data za msingi zilipatikana kwa mbinu ya kielektroniki na kimaktaba. Uchambuzi na mjadala wa data uliongozwa na Nadharia  ya Semiotiki. Msingi mkuu wa nadharia hii ni kushughulika na ishara pamoja na uashiriaji katika kazi za fasihi. Matokeo ya  utafiti yamewasilishwa kwa mbinu ya kimaelezo. Matokeo yameonesha namna msuko wa fantasia katika kitabu teule unaivyoibua  dhamira zinazolenga kuifunza, kuiimarisha na kuiweka jamii pamoja katika misingi imara ya utamaduni, siasa na uchumi. Dhamira  zilizoibuliwa zinawasilisha matendo ya msingi ya binadamu yanayojidhihirisha katika nyanja zote za maisha na maendeleo yake. Kwa  hiyo, makala hii inapendekeza kuwa utafiti ufanyike zaidi katika tanzu za fasihi simulizi ya Kiswahili kuhusu matumizi ya fantasia  yanavyofumbata masuala ya uchumi, siasa, utamaduni, falsafa na itikadi za jamii.
Gerephace Mwangosi Copyright (c) 2025 2025-01-16 2025-01-16 22 1 112 122 Mtindo wa Usambamba katika Utenzi wa Seyidina Ali na Mudhari bin Darimi https://www.ajol.info/index.php/kcl/article/view/286673
Katika makala hii tumechunguza aina mbalimbali za usambamba na mchango wake katika Utenzi wa Seyidina Ali na Mudhari bin Darimi. Ili kufanikisha hili, makala imeongozwa na Nadharia ya Umitindo ambayo inachunguza na kutoa fasiri kwa kazi za isimu na fasihi. Nadharia hii imetumika katika makala hii kwa kuwa uchunguzi wa vipengele vya kifasihi hutegemea vile vya kiisimu. Nadharia ya Umitindo inahusishwa na Geoffrey Leech (1969) hasa katika andiko lake la A Linguistic Guide to English Poetry. Lengo la uhakiki wetu ni kuweka wazi aina mbalimbali za usambamba zinazobainika katika utenzi huu na michango yake katika kufanikisha fani na maudhui kwenye utungo huu. Kutokana na uchunguzi wetu, tumebainisha kuwa matumizi ya usambamba kama aina ya urudiaji yanachangia  katika ukuzaji na uendelezaji wa dhamira, usawiri na ujenzi wa wahusika na kuingiliana na sifa nyingine za kimtindo ili kuibua umbuji wa  kijumla wa utungo huu.
Adria Fuluge Copyright (c) 2025 2025-01-16 2025-01-16 22 1 123 136 Gathoni’s Aggression in Ngugi wa Thiong’o and Ngugi Wa Mirii’s Play Nitaolewa Nikipenda: A Representation of Africa’s Desired Political, Social and Economic Autonomy https://www.ajol.info/index.php/kcl/article/view/286674
This paper was guided by the Post-colonial Theory with a focus on Frantz Fanon’s leanings on life aspects of the formerly colonised Africans. It was also guided by African Feminism in its analysis and discussion of the findings. It is based on Frantz Fanon’s ideas and arguments contained in his book The Wretched of the Earth (1965). Some of the ideas contained in this book were used as lenses to  discuss Ngugi wa Thiong’o and Ngugi wa Mirii’s Kiswahili translation of their play I Will Marry When I Want (1982) translated as Nitaolewa Nikipenda (1982). It singles out Gathoni, a female character in the play who, throughout the story line, is projected as potentially  aggressive, independent minded and as a character who does not allow others to manipulate her in any way. Together with Fanon’s  perspectives on Africans’ liberation and African Feminism literary lenses, this paper argues that, Gathoni sharply contrasts with a  traditional African woman who has been projected in literary works as docile, unassertive and who depends on others especially men for  her welfare. This work was a library-based study whose data were collected through close reading of both play versions; that is the  Kiswahili and the English version to facilitate easy translation of the quotations. These were the primary data. The review of different  documents including journal articles and dissertations both as hard copy and soft copy materials on the internet generated the  secondary data. The findings reveal that, Gathoni’s aggression and independent mindedness is the writers’ representation or projection  of social, economic and political freedom that they would aspire the formerly colonised Africans to possess.
Emmanuel Kilatu Copyright (c) 2025 2025-01-16 2025-01-16 22 1 137 148 Mkengeuko wa Malezi kwa Wahusika katika Riwaya ya Rosa Mistika https://www.ajol.info/index.php/kcl/article/view/286675
Makala hii imechunguza mkengeuko wa malezi wa wahusika katika riwaya ya Rosa Mistika. Data za makala zimepatikana maktabani kwa mbinu ya usomaji makini wa matini ya riwaya husika na kisha kuchambua data hizo kwa mkabala wa kimaudhui na kuziwasilisha kwa  mkabala wa kitaamuli. Makala imeongozwa na misingi ya Nadharia ya Sosholojia ya Kifasihi katika ukusanyaji na uchambuzi wa data.  Matokeo yanaonesha kuwapo kwa matukio mengi ya wahusika kukengeuka malezi katika riwaya hii. Matukio hayo ni ubakaji, kujiua, rushwa, umalaya, kupuuza ushauri na matusi. Matukio haya yameoneshwa katika kazi husika kwa kuwa ni mwakiso wa uhalisi wa kijamii  kama Nadharia ya Sosholojia ya Kifasihi inavyofungamanisha jamii na kazi za fasihi.
Selestino H. Msigala Copyright (c) 2025 2025-01-16 2025-01-16 22 1 149 163