https://www.ajol.info/index.php/kcl/issue/feed Kioo cha Lugha 2024-04-12T13:23:49+00:00 Dkt. Rhoda Peterson Kidami kidamis@yahoo.com Open Journal Systems
Kioo cha Lugha is an international journal published by the Institute of Kiswahili Studies (IKS). The journal is devoted to the publication of papers on Kiswahili language, linguistics and literature and other African languages. It promotes critical discussions and reviews, especially on contemporary issues regarding language and literature. The journal also publishes short pieces of fiction and poems. It is published annually but from 2021 it will be published bi-annually.

Journal website: https://journals.udsm.ac.tz/index.php/kcl

https://www.ajol.info/index.php/kcl/article/view/268389 Dhima ya Miiko katika Uibuaji wa Maudhui katika Fasihi ya Kiswahili: Mifano kutoka Riwaya ya Bw. Myombekere na Bi. Bugonoka Ntulanalwo na Bulihwali 2024-04-12T11:44:02+00:00 Atupele Kamage kamageamkei@yahoo.com Edith B. Lyimo kamageamkei@yahoo.com
Makala hii inajadili dhima ya miiko katika uibuaji wa maudhui katika fasihi ya Kiswahili. Shabaha kuu ni kubainisha jinsi miiko ilivyo na dhima katika uibuaji wa maudhui mbalimbali katika jamii. Makala hii imetokana na madai ya baadhi ya tafiti zilizotangulia kueleza  kwamba miiko ni imani za kishirikina (Frazer, 1940; Smith, 1961; Fielding, 1966) na inatumika katika jamii ambazo ziko nyuma katika  masuala ya kisayansi (Madumulla, 1988). Kutokana na mitazamo hiyo, tuliona ipo haja ya kuchunguza dhima ya miiko katika uibuaji wa  maudhui kwa wanajamii kupitia riwaya ya Kiswahili. Ili kutimiza azma hii riwaya ya Bw. Myombekere na Bi. Bugonoka Ntulanalwo na  Bulihwali ilichunguzwa. Uchambuzi wa data uliongozwa na Nadharia ya Ontolojia ya Kiafrika. Matokeo ya uchunguzi katika makala hii yamebaini kuwa miiko katika fasihi ya Kiswahili ina dhima ya kuelezea maudhui mbalimbali. Baadhi ya maudhui hayo ni maadili, mahusiano ya jamii, afya, imani za kijamii, thamani ya kazi na umuhimu wa kutunza mazingira. Miiko hiyo husawiriwa ndani ya jamii na  kuakisi uhalisi wa maisha katika miktadha mbalimbali ya kijamii, kiutamaduni, kijiografia na ulimwengu kwa ujumla.
2024-04-12T00:00:00+00:00 Copyright (c) 2024 https://www.ajol.info/index.php/kcl/article/view/268391 Matumizi ya Mandhari za Kifasihi Simulizi katika Ujenzi wa Dhamira za Ushairi Andishi: Mifano kutoka Diwani za Muhammed Seif Khatib 2024-04-12T11:48:46+00:00 Baraka Sikuomba 1987baraka@gmail.com Joviet Bulaya 1987baraka@gmail.com
Makala hii inakusudia kuchunguza jinsi mandhari za fasihi simulizi zilivyotumika kujenga dhamira katika diwani za Fungate ya Uhuru (1988), Wasakatonge (2003) na Vifaru Weusi (2016). Sababu ya  uchunguzi huu ni kwamba mandhari ni kipengele muhimu cha fani  katika  ujenzi wa kazi za fasihi andishi kama vile riwaya, tamthiliya na  hadithi fupi kuliko utanzu wa ushairi. Data za makala hii  zilikusanywa  kwa kutumia mbinu ya usomaji makini. Nadharia ya Mwitiko wa  Msomaji iliyoasisiwa na Wolfgang Iser (1978), Stanley Fish  (1980),  James Tompkins (1980), Haus Robert Jauss (1982) na Robert Holub  (1984) ndiyo iliyoongoza ukusanyaji na uchambuzi wa data za  makala hii. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa kuna matumizi ya mandhari  za fasihi simulizi katika kujenga dhamira. Dhamira hizo ni  matabaka,  ushujaa na ujasiri, ukombozi wa kifikra, kutoheshimu taaluma na uzalendo wa kweli.
2024-04-12T00:00:00+00:00 Copyright (c) 2024 https://www.ajol.info/index.php/kcl/article/view/268394 Mdhihiriko wa U-Naijeria katika Video za Nyimbo za Muziki wa Kizazi Kipya nchini Tanzania 2024-04-12T12:11:19+00:00 Gervas A. Kasiga kassiga@googlemail.com
Makala hii inajadili mdhihiriko wa U-Naijeria katika video za nyimbo za muziki wa kizazi kipya wa Kiswahili nchini Tanzania. Utafiti wa makala hii uliendeshwa kitaamuli. Makala ilitumia usanifu wa kifenomenolojia, ambapo tafakuri ilikuwa ni kiini katika kuhusisha na kutoa  majawabu ya taarifa mbalimbali zilizochunguzwa. Misingi ya Nadharia ya Uhalisia ilitumika katika ukusanyaji na uchambuzi wa data za  utafiti wa makala. Katika uainishaji wa matokeo ya utafiti, mdhihiriko wa U-Naijeria katika video za nyimbo za muziki wa kizazi kipya wa  Kiswahili nchini Tanzania ulibainika katika vipengele vya mavazi, ala na midundo ya muziki, mitindo ya kiuchezaji, mandhari, utumiwaji wa  vifaa vya kijukwaa na matumizi ya lugha. Mwisho, imependekezwa kuwa ni muhimu kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya wa  Kiswahili nchini Tanzania kuhusisha vipengele vya utamaduni katika uundaji wa video zao ili kuwezesha ukuzaji wa sanaa, mila, desturi na  maadili ya Kitanzania.
2024-04-12T00:00:00+00:00 Copyright (c) 2024 https://www.ajol.info/index.php/kcl/article/view/268395 Relevance of the Portrayal of Masculinity in Ebrahim Hussein’s Plays to the Tanzanian and Kenyan Societies 2024-04-12T12:16:16+00:00 Yohana Makeja John yohana.john@out.ac.tz
This paper examines the relevance of the portrayal of masculinity in  Ebrahim Hussein’s Kinjeketile and Kwenye Ukingo wa Thim, in  response to the scholarly need to establish the relevance of the literary  portrayal of masculinity in the plays to the Tanzanian and Kenyan  societies. The study is qualitative and adopts Butler’s (1990) Gender Performativity Theory and Connell’s (1995) Gender Order  Theory that  were both used as a framework for reading, analyzing and interpreting  characters’ expressions and performances of  masculinity in the  selected readings. A Constructivist Paradigm was employed, and it  comprised of a number of stages, namely  identification of the plays as  the primary texts, a close reading of the plays and a review of literature  on the gendered portrayals in  Hussein’s plays. The researcher finally  found that the dramatic portrayal of masculinity in Hussein’s  Kinjeketile and Kwenye Ukingo wa  Thim is realistic and relevant to the  Tanzanian and Kenyan societies. Therefore, the present study is very  significant since it gives  significant knowledge of the reality and  relevance of the two dramatic works of art to the Tanzanian and  Kenyan societies with regard to  the dramatic portrayal of masculinity  in them. The study fills the knowledge gap of the relevance of the literary portrayal of the master- servant relationship between  Tanganyikans and the Germans from 1890 to 1904 and the famous  1987 Kenyan ‘Otieno case’, and how  masculinity was represented both  positively and negatively in both cases.
2024-04-12T00:00:00+00:00 Copyright (c) 2024 https://www.ajol.info/index.php/kcl/article/view/268397 Usawiri wa Nduni za Shujaa katika Kisakale cha Munyigumba wa Jamii ya Wahehe 2024-04-12T12:30:04+00:00 Aneth W. Kasebele aneth.kasebele@muce.ac.tz
Makala hii inachunguza usawiri wa nduni za shujaa katika Kisakale cha Munyigumba wa jamii ya Wahehe. Watafiti wa masuala ya nduni za shujaa wa Kiafrika wanaeleza kuwa kila jamii ina nduni zake za shujaa zinazotegemea mtazamo, falsafa na utamaduni wa jamii husika. Hivyo, si rahisi kwa jamii zisizo na uhusiano wa karibu kuwa na nduni za shujaa zinazolandana katika hali zote. Kuwapo kwa mitazamo na tamaduni tofautitofauti kunasababisha sifa za shujaa wa jamii moja kuwa tofauti na za shujaa anayepatikana katika jamii nyingine. Hivyo, kilichofanyika katika makala hii ni kubainisha nduni za shujaa wa jamii ya Wahehe ili kufahamu nduni zake. Makala hii imeongozwa na mawazo ya Nadharia ya Ontolojia ya Kiafrika kwa kuwa shujaa anayechunguzwa anatoka katika jamii za kijadi za Kiafrika. Data za makala  hii zimekusanywa kwa njia ya usaili na uchambuzi matini kutoka katika vijiji vya Kalenga na Rungemba, Mkoani Iringa. Matokeo ya utafiti  wa makala hii yameonesha kuwa shujaa wa jamii ya Wahehe ana nduni mbalimbali zilizothibitika kupitia Kisakale cha Munyigumba.  Aidha, imethibitika kuwa, jamii mbalimbali za Kiafrika zina mfanano mkubwa unaosababisha hata mashujaa wake kuwa na nduni  zinazofanana kwa kiasi kikubwa.
2024-04-12T00:00:00+00:00 Copyright (c) 2024 https://www.ajol.info/index.php/kcl/article/view/268399 Nafasi ya Biashara za Kimataifa katika Kukuza Uzungumzaji wa Kiswahili kwa Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Rwanda 2024-04-12T12:36:13+00:00 Emmanuel Niyirora e.niyirora@ur.ac.rw Wallace K. Mlaga e.niyirora@ur.ac.rw
Tafiti zinaonesha kwamba lugha ya Kiswahili nchini Rwanda  haizungumzwi vizuri kama lugha nyingine zinazofundishwa nchini  humo.  Ingawa lugha hii haizungumzwi kwa ufasaha, hasa katika shule  za sekondari, wanafunzi wanaojifunza katika baadhi ya shule za  sekondari wanapata fursa ya kuchangamana na wazungumzaji wa  Kiswahili. Wazungumzaji hao ni pamoja na wazazi, jamaa na marafiki wanaofanya biashara za kimataifa za kuvuka mpaka. Jambo hili  husaidia sana katika uimarishaji wa Kiswahili miongoni mwa  wanafunzi.  Makala hii ililenga kutimiza malengo mahususi mawili.  Lengo la kwanza lilikuwa kujadili dhana ya biashara za kimataifa za  kuvuka  mpaka na dhana ya uzungumzaji wa Kiswahili na lengo la pili  lilikuwa kubainisha mchango wa biashara za kimataifa za kuvuka  mpaka  katika uimarishaji wa uzungumzaji wa Kiswahili kwa  wanafunzi wa shule za sekondari nchini Rwanda. Utafiti uliongozwa na Nadharia ya  Utamaduni Jamii. Mbinu za uchanganuzi wa matini na  mahojiano zilitumiwa kukusanya data. Usampulishaji lengwa ulitumiwa kupata  sampuli ya utafiti kutoka kwenye shule zilizoteuliwa.  Matokeo ya utafiti yameonesha kuwa biashara za kimataifa za kuvuka  mpaka zina  mchango mkubwa katika uimarishaji wa uzungumzaji wa  Kiswahili kwa wanafunzi wa shule za sekondari nchini Rwanda.  Isitoshe, utafiti  huu umependekeza kuwa walimu wanapaswa kutumia  fursa ya biashara za kimataifa za kuvuka mpaka katika uimarishaji wa  Kiswahili  miongoni mwa wanafunzi wao.
2024-04-12T00:00:00+00:00 Copyright (c) 2024 https://www.ajol.info/index.php/kcl/article/view/268401 Uhawilishwaji wa Wakaa wa Kihehe na Athari zake katika Ujifunzaji wa Kiswahili Sanifu kama Lugha ya Pili 2024-04-12T12:49:13+00:00 Mwaija Ngenzi mwaijangenzi2@gmail.com
Makala hii imechunguza uhawilishwaji wa wakaa wa Kihehe na athari zake katika ujifunzaji wa Kiswahili kama lugha ya pili. Lengo kuu ni kuchunguza namna uhawilishwaji wa wakaa wa Kihehe katika lugha ya Kiswahili unavyoiathiri lugha hiyo. Data zilikusanywa kutoka kwa wajifunzaji wa lugha ya Kiswahili wa jamii ya Wahehe na walimu wa somo la Kiswahili kwa kutumia mbinu za masimulizi ya hadithi na usaili. Uchambuzi wa data uliongozwa na Nadharia ya Usasanyuzi Linganishi. Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa uhawilishwaji wa  wakaa wa Kihehe katika Kiswahili husababisha athari katika lugha hiyo. Athari iliyobainika ni mabadiliko ya matamshi ya maneno mbalimbali ya Kiswahili ambayo husababisha ubadilishaji wa maana msingi za maneno husika. Ili kuondoa au kupunguza athari hiyo, makala hii imependekeza uelimishaji wa jamii za vijijini kuhusu umuhimu wa lugha ya Kiswahili. Pia, serikali iandae walimu wa kutosha  ambao ni wabobezi wa kufundisha Kiswahili kama lugha ya pili.
2024-04-12T00:00:00+00:00 Copyright (c) 2024 https://www.ajol.info/index.php/kcl/article/view/268402 Matumizi ya Nahau katika Ujarabati wa Mikakati ya Kisintaksia ya Usimbaji wa Fokasi katika Sentensi za Kiswahili 2024-04-12T13:07:05+00:00 Elishafati J. Ndumiwe ndumiweelisha@gmail.com Amani Lusekelo ndumiweelisha@gmail.com
Usimbaji wa fokasi katika sentensi za lugha za Kibantu hufanyika kwa kutumia mikakati mbalimbali ya kimofolojia, kisintaksia au  kifonolojia (van der Wal, 2009; Yonenda, 2011; Morimoto, 2014; Ndumiwe,  2023). Aidha, kuna mbinu tofautitofauti zinazotumika  kung’amua  ikiwa mikakati madhukura inasimba fokasi au la. Mojawapo ya mbinu  hizo ni matumizi ya nahau. Van der Wal (2016, 2021)  alichunguza  mbinu hiyo katika ung’amuzi wa usimbaji wa fokasi katika lugha za  Kimakua (P31), Kizulu (S42), Kimatengo (N13), Kirundi  (JD62),  Kichangana (S53), Kiganda (JE15), Kinyakyusa (M31), Kibukusu  (JD31c) na Kitharaka (E54). Hata hivyo, hakuna utafiti uliofanyika  katika lugha ya Kiswahili (G42) kuhusu matumizi ya nahau katika  ujarabati wa mikakati ya usimbaji wa fokasi. Kwa hiyo, lengo la  makala  hii ni kuhakiki mikakati ya kisintakisa ya usimbaji wa fokasi  kwa kutumia nahau za Kiswahili. Data zimekusanywa kwa kutumia  mbinu za  usaili na upitiaji wa nyaraka. Data hizo zimechambuliwa  kitaamuli kwa kuongozwa na Nadharia ya Vibadala vya Kisemantiki  (Rooth,  2016). Utafiti huu umebainisha kuwa nahau za Kiswahili  zikiundiwa sentensi kwa kutumia mikakati ya ukasimishaji, upinduzi  wa  viambajengo na utenguaji kushoto, maana ya nahau inatoweka.  Kwa hiyo, utowekaji wa maana ya nahau huthibitisha kuwa mikakati    husika hutumika kusimba fokasi katika lugha ya Kiswahili.
2024-04-12T00:00:00+00:00 Copyright (c) 2024 https://www.ajol.info/index.php/kcl/article/view/268403 Examining the Communicative Value of Sign X in the Public Space in Tanzania: The Case of Swahili Context 2024-04-12T13:18:37+00:00 Paschal C. Mdukula pcharles@udsm.ac.tz
This paper investigates the multifaceted communicative value of sign X in the Swahili context in Tanzania, encompassing both physical  and virtual spaces. Cities around us are marked by many semiotic signs which present different communication cues and experiences.  These signs are imagery symbols which are assigned meaning by the people who use them to communicate different concepts, ideas,  beliefs and experiences. To dissect the diverse connotations associated with sign X as it operates within Tanzania’s Swahili context, this  study used two distinct datasets: narrative data sourced from survey questionnaires completed by a cohort of 103 participants and  collection of 47 photographic data featuring sign X that were captured through digital camera across the physical and virtual public  spaces. The study employed Socio-Semiotic Theory to analyse the communicative value of sign X in the studied public space. The theory  focuses on how meanings are constructed and communicated through various signs and symbols within Swahili context in Tanzania. The  study findings revealed that sign X was employed to communicate multiple meanings in the Swahili context. These include warnings,  prohibitions, calls for demolition, removal instructions, misinformation and fake news, cancellations, deletions, hidden value, protocols to  observe, marker of death, expression of love and sexuality, and poignant reminders of personal experiences from the past.
2024-04-12T00:00:00+00:00 Copyright (c) 2024