Main Article Content

Nadharia ya Ubaada-ukoloni katika Tamthilia ya Amezidi (1995) ya S. A. Mohamed


ZL Daniel

Abstract

Makala haya yanaonesha nadharia ya Ubaada-ukoloni jinsi inavyojidhihirisha katika tamthilia ya Amezidi. Katika uchambuzi huu, nadharia hii inafafanuliwa kwa undani kwa kuangalia waasisi wake, mawazo makuu ya nadharia hii kwa ujumla pamoja na ujitokezaji wa nadharia hii katika kazi za fasihi. Makala haya yanachambua kwa undani pia namna mawazo makuu ya nadharia ya Ubaada-ukoloni yanavyojitokeza katika tamthilia ya Amezidi. Mawazo hayo yanaelezwa kwa kutumia hali za kiuchumi, kisiasa na kijamii ambazo zinabainishwa na mwandishi wa tamthilia ya Amezidi.

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X