Main Article Content
Dhana ya Uambikaji katika Kiswahili
Abstract
Lugha ya Kiswahili inaunda msamiati wake kwa kutumia njia mbalimbali ili kukidhi haja ya mawasiliano. Miongoni mwa njia zinazotumika kuunda msamiati huo ni pamoja na uambishaji na unyambulishaji. Katika Kiingereza njia hizi zinaelezwa kwa urahisi na zinaeleweka. Hali ni tofauti katika Kiswahili. Makala haya yanafafanua dhana hizi, na kwa kutumia dhana ya uambikaji inajadili uhusiano uliopo baina yake. Pili, kwa kutumia mifano na maelezo kuntu kutoka katika Kiswahili, makala yanapendekeza dhana ya uambikaji (Affixation) kutumika kama msingi wa kuonesha uhusiano huo ili kuondoa mkanganyiko uliopo.