Main Article Content
Mbinu Mbalimbali za Kutathmini Tafsiri
Abstract
Makala haya yanajadili mbinu mbalimbali za kutathmini tafsiri katika muktadha wa tafsiri za Kiswahili na lugha nyingine za Tanzania. Madai makuu ya makala haya ni kwamba tafsiri hufanyiwa tathmini katika hatua zake mbalimbali. Tathmini katika tafsiri1 inaweza kufanyika mwanzo (yaani, kabla ya kuanza kutafsiri), katikati ya mchakato wa kutafsiri na mwishoni (yaani, baada ya tafsiri kufanyika). Tathmini inaweza kufanyika kwa kutumia mbinu ya kulinganisha matini, kufanya tafsiri rejeshi, mbinu ya kupima uelewa, kupima usomekaji na kupima uasili. Madai ya makala haya ni kwamba mbinu hizi hutumika kutegemeana na aina ya tathmini inayofanyika. Aidha, mbinu zaidi ya moja zinaweza kutumika katika kutathmini tafsiri moja. Kupitia tathmini, tafsiri zimekuwa zikiboreshwa kila mara, na hata wanazuoni wamekuwa wakiibua mikakati na mbinu mpya za kuboresha mchakato wa kutafsiri.