Main Article Content

Ufundishaji wa Kusoma na Kuandika Kiswahili: Uzoefu wa Idara ya Lugha na Taaluma za Kiafrika, Chuo Kikuu cha Sebha, Libya


IH Elmahdi

Abstract

Makala haya yanahusu shughuli za kufundisha Kiswahili kama lugha ya kigeni katika Chuo Kikuu cha Sebha nchini Libya. Kwanza inaeleza historia ya Kiswahili – yaani kilianza lini kufundishwa kwa madhumuni gani na nani walikuwa wanzilishi. Halikadhalika makala ya naeleza utaratibu uliowekwa na idara ili kuweza kufundisha stadi hizi kama sehemu ya kumfundisha mwanafunzi kuandika kwa hati ya Kirumi na wakati huohuo kumsaidia kuimarisha ujuzi wake wa Kiswahili. Matatizo na mbinu za kuyatatua na mafanikio yaliyopatikana yanaelezwa pamoja na mustakabali uliopo wa Kiswahili katika Idara ya Lugha na Taaluma za Kiafrika, Chuo Kikuu cha Sebha nchini Libya.

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X