Main Article Content

Falsafa ya Maisha katika Ushairi wa Mugyabuso Mulokozi na Shaaban Robert


A Mnenuka

Abstract

Kutofautiana kimawazo ni miongoni mwa sifa muhimu sana za binadamu. Sifa hii inasahauliwa na watu wengi kiasi cha kuwafanya washangae inapotokea watu wakiwa na mawazo yanayotofautiana. Binadamu ana akili inayoweza kubuni vitu mbalimbali vinavyokubalika na wengi au vinavyokubalika na baadhi tu ya watu. Tofauti za binadamu hujitokeza katika maeneo mbalimbali mojawapo ni katika kazi za kubuni ambapo mtunzi wa kazi anaweza kueleza hisia na mawazo yake au kuwakilisha mawazo ya watu wengine kulingana na matakwa yake. Makala haya yanachunguza mitazamo kuhusu dhana ya maisha na mustakabali wake kama inavyoelezwa na Shaaban Robert na Mugyabuso Mulokozi. Tutachunguza ili kubaini kufanana na kutofautiana kwa mitazamo yao. Aidha, makala yataeleza chanzo na misingi ya tofauti hizo, pamoja na kufanana kwao.

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X