Main Article Content
Dhima ya Kibwagizo katika Ushairi wa Kiswahili
Abstract
Makala haya yanatathmini dhima ya kibwagizo katika ushairi wa Kiswahili. Baadhi ya wahakiki wa utanzu huu wamekuwa wakitoa maelezo ya kijumla kuhusu uwiano uliopo kati ya kibwagizo cha shairi na maudhui yanayowasilishwa. Maelezo hayo yanaibua utata katika fasili na maana ya mshororo huo ujulikanao kama kibwagizo. Hali hii inaonesha kwamba matumizi ya kibwagizo bado hayajashughulikiwa ipasavyo. Katika makala haya, kibwagizo kimefafanuliwa kwa namna kinavyoweza kusaidia kuibua umbo, muundo, kuelekeza mtindo na ridhimu au mahadhi katika ushairi wa Kiswahili. Aidha, makala yanadhukuru namna kibwagizo kinavyoweza kutumiwa katika uainishaji wa mashairi.