Main Article Content
Dhima ya Mwingilianomatini kwenye Hadithi za Watoto katika Kiswahili
Abstract
Wasimulizi na waandishi wa fasihi ya Kiswahili kwa watoto, wamekuwa wakitumia mtindo wa kuchanganya vipengele mbalimbali vya kisanaa katika kazi moja. Mbinu hii inatazamwa na makala haya kuwa ni mwingilianomatini katika fasihi. Mathalani, mwandishi anayeandika au kusimulia hadithi za Kiswahili hasa za watoto, hujikuta akichanganya matini za nyimbo, semi, hadithi ndani ya hadithi, maigizo, matumizi ya ishara na kadhalika. Kuchanganya huko kwa vipengele tofauti katika kazi moja ni kitu ambacho kimezoeleka sana miongoni mwa wanafasihi. Makala haya yana lengo la kubainisha dhima mbalimbali za vipengele hivyo kuingiliana.