Main Article Content

Kiswahili na Usalama wa Chakula: Vikwazo vya Lugha


NJ Ngowa
S Ryanga

Abstract

Kufanikisha usalama wa chakula kunategemea ufahamu wa wakulima na jamii ya mashambani1 kuhusu dhana ya usalama wa chakula, na jinsi inavyojikita katika maeneo yao kimazingira, kimila na kiutamaduni. Uelewa wa wakulima si wa kiutaaluma tu bali pia lugha inayotumika kama inatosheleza mahitaji yao ya ufahamu wa dhana zinazotumiwa, jinsi zinavyofunzwa na kuhusishwa na utamaduni wa jamii zinazohusika. Lugha ina nafasi kubwa katika uhamasishaji na usambazaji wa habari, ujuzi na teknolojia kwa jamii. Lakini lugha haitendi kazi katika ombwe. Lugha hujikita katika utamaduni, mila na uzoefu wa jamii. Hivyo lugha huongoza falsafa, ufahamu na jinsi watu wanavyofasiri ulimwengu wao kijamii, kiuchumi, hata kisiasa. Lugha inayotumika kuhamasisha wakulima, ugumu wa istilahi na dhana ngeni katika harakati za kupata usalama wa chakula na kuondoa umaskini huzua mielekeo na misisimko tofauti kuhusu upokezi ama upuuzaji wa ujuzi na teknolojia mpya. Hii ni kwa sababu ujuzi mpya na dhana ngeni lazima zieleweke kwa wapokezi na zirejelee na kuwiana na falsafa na mila za wanaofunzwa ujuzi na teknolojia hiyo. Huwezi kulazimisha matumizi ya ujuzi na dhana mpya kwa jamii isiyofahamu maana na umuhimu wake.

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X