Main Article Content

Kiswahili kama Nyenzo ya Maendeleo Nchini Kenya


M Mukuthuria

Abstract

Ukuzaji na uendelezaji wa Kiswahili kama lugha ya taifa nchini Kenya ni lengo la taifa ambalo bado halijapewa kipaumbele kinachostahili. Hata hivyo, tangu Kenya ilipojinyakulia uhuru, matumizi ya lugha hii yamepevuka kinyume na matarajio ya wengi, kiasi kwamba, kwa sasa, mchango wake katika kufanikisha maendeleo ya sehemu za mashambani1 hauwezi kukadiriwa. Nia ya makala haya ni kubainisha mchango huu katika kufanikisha malengo ya kitaifa katika sehemu za mashambani. Ili kufanikisha lengo la makala haya, kielelezo cha nadharia ya mawasiliano kinachotilia maanani hali halisi ya sehemu za mashambani Kenya kitatumika. Lengo kuu ni kuthibitisha jinsi ambavyo mikakati ya kukuza Kiswahili, kama lugha ya kutegemewa katika nyanja zote, haiwezi kuepukika hasa katika kipindi hiki ambacho jitihada za kuunda Jumuiya ya Afrika Mashariki zimeshika kasi. Mwisho makala yameainisha vikwazo vinavyokikumba Kiswahili katika maeneo haya ya mashambani pamoja na kutoa mapendekezo ya kudhibiti na kuimarisha lugha hii kama nyenzo ya maendeleo sehemu za mashambani na katika taifa la Kenya kwa ujumla.

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X