Main Article Content

MCHANGO WA MWALIMU J.K. NYERERE KATIKA TAFSIRI NA MAENDELEO YA LUGHA


H.J.M Mwansoko

Abstract

Kwa kuzingatia tafsiri mbili za J.K. Nyerere, Julius Kaizer (1963) na Mabepari wa Venus (1969), makala inaeleza: (i) kwa nini Mwalimu Nyerere alitafsiri maandishi ya Shakespeare, (ii) ufanisi wa tafsiri zake, na (iii) mchango wa tafsiri hizo. Makala inaonyesha kuwa tafsiri hizo zinazingatia mbinu za kisemantiki zaidi kuliko mbinu nyingine ingawa hapa na pale mbinu ya kimawasiliano inatumika pia. Makala inataja mchango wa tafsiri hizo kuwa ni kukuza fasihi ya Kiswahili, kukuza msamiati na kuwatia ari wafasiri wengine.

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X